tangazo

tangazo

Tuesday, January 27, 2015

JUMLA YA SKULI 21 ZA SEKONDARI ZIMEJENGWA NA SERIKALI YA MAPINDUZI YA ZANZIBAR



ZANZIBAR.
Jumla ya skuli  21  za sekondari zimejengwa na Serikali ya Mapinduzi ya ZanziBar kwa kushirikiana na Benki ya Dunia na Benki ya Kiarabu kwa Maendeleo ya Afrika (Badea)
 HAYO  YAMEELEZWA Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali ZANZIBAR Zahra Ali Hamad  wakati AJIBU MASWALI YA WAJUMBE WA BARAZA LA WAWAKILISHI katika  KIKAO CHA BARAZA HILO  KINACHOENDELEA HUKO Chukwani NJE KIDOGO YA MJI WA ZANZIBAR.
Bi. Zahra amemuhakikishia Mwakilishi huyo kwamba mpango wa kujenga skuli ya ghorofa katika eneo la skuli hiyo upo kutokana na kubainika kuwepo kwa idadi kubwa ya wanafunzi katika mitaa ya karibu na skuli hiyo.
 AMEsema kuwa LICHA YA utekelezaji wa mpango  huo,  Serikali ya Mapinduzi Zanzibar kwa kushirikiana na mfuko wa OPEC inakusudia kujenga skuli kumi  10 za ghorofa ambapo mradi huo ulichelewa kuanza kutokana na kutokamilika  taratibu za kisheria kuhusu makubaliano ya mkopo.
 Wakati huo huo Wizara ya Ardhi, Makaazi, Maji na Nishati  inakusudia kumaliza  tatizo la upatikanaji wa huduma Ya maji ifikapo mwaka 2017 kwa Wananchi wa Mji mkogwe na Ng’ambu.
Hayo yameelezwa na Naibu  Waziri wa wizara hiyo   Haji Mwadini Makame wakati akijibu MASWALI YA WAJUMBE WA BARAZA LA WAWAKILISHI ZANZIBAR.
Amesema kuwa wanakusudia kumaliza tatizo kwa kuimarisha huduma hiyo kwa kuimarisha miundo mbinu ikiwemo kubadilisha  Mabomba ya zamani  ambayo yamechoka na kushindwa kuhimili ongezeko kubwa la wahamiaji.
Aidha aMEBAINISHA  kuwa hali ya upatikanaji wa maji katika Mkoa wa Mjini inaendelea kuimarika siku hadi siku ambapo kuna baadhi ya maeneo yanapata Maji kwa muda mrefu na mengine yanapata maji kwa mgao hasUSAN wakati wa kiangazi  na maeneo machache hukosa kabisa.
AMESema  KUWA kupitia Mamlaka ya maji wamekuwa wakifanya juhudi kutafuta  ufumbuzi  wa suala hilo ikiwa ni pamoja na  uchimbaji wa Visima  vipya katika maeneo mbali mbali.                                

No comments:

Post a Comment