tangazo

tangazo

Wednesday, January 7, 2015

COMORO NA ZANZIBAR ZAENDELEZA MASHIRIKIANO



ZANZIBAR.

RAIS WA ZANZIBAR DK. ALI MOHAMED SHEIN AMESISISTIZA KUWA ZANZIBAR ITAENDELEZA UHUSIANO NA USHIRIKIANO WA KIHISTORIA ULIOPO KATI YAKE NA COMORO HASUSAN KATIKA UIMARISHAJI WA SEKTA ZA MAENDELEO NA UTAMADUNI.

DK. SHEIN AMEYASEMA HAYO WAKATI ALIPOFANYA MAZUNGUMZO NA BALOZI WA COMORO NCHINI TANZANIA DK. AHMADA EL BADAOUI MOHAMED, IKULU MJINI ZANZIBAR.

KATIKA MAZUNGUMZO HAYO DK. SHEIN AMESEMA KUWA ZANZIBAR INAJIVUNIA UHUSIANO NA USHIRIKIANO HUO WA MUDA MREFU SAMBAMBA NA MAINGILIANO NA UHUSIANO WA WATU WAKE KATI YA NCHI MBILI HIZO AMBAPO WAMEWEZA KUIMARISHA UDUGU WAO WA KIHISTORIA.

KUTOKANA NA HATUA HIYO, DK. SHEIN AMESEMA KUWA MASHIRIKIANO KATIKA UIMARISHAJI WA SEKTA ZA MAENDELEO SAMBAMBA NA UTEKELEZAJI WA MKATABA WA MAKUBALIANO ULIOTIWA SAINI MWAKA JANA WAKATI WA  ZIARA YAKE ALIYOIFANYA NCHINI HUMO UTASAIDIA KUIMARISHA JUHUDI HIZO.

DK. SHEIN ALISEMA KUWA UTEKELEZAJI WA MAKUBALIANO HAYO UTASAIDIA KWA KIASI KIKUBWA KUIMARISHA USHIRIKIANO KATI YA ZANZIBAR NA COMORO AMBAO UMEWEZA KUKUZA UDUGU MIONGONI MWA WATU WAKE.

NAE BALOZI WA COMORO NCHINI TANZANIA DK. AHMADA EL BADAOUI MOHAMED AMESEMA KUWA COMORO INATHAMINI SANA UHUSIANO NA USHIRIKIANO WA MUDA MREFU KATI YAKE NA ZANZIBAR AMBAO NCHI YAKE UMEAHIDI KUUDUMISHA KWA MANUFAA YA PANDE ZOTE MBILI.

BALOZI HUYO ALISEMA KUWA COMORO NA ZANZIBAR INA HISTORIA KUBWA KATIKA KUTOA ELIMU HASUSAN YA DINI YA KIISLAMU NA KUELEZA KUWA MASHEKHE WENGI WAKUBWA WA COMORO ELIMU YAO HIYO WAMEIPATA  ZANZIBAR AKIWEMO BABA YAKE MZAZI.

No comments:

Post a Comment