WILAYA YA MJINI.
WAUMINI WA DINI TAKIISLAM KOTE NCHINI WAMETAKIWA
KUJITAHIDI KUTEKELEZA MAFUNDISHO YA MTUME MUHAMMAD (S.A.W) KATIKA MAISHA YAO
ILI KUPATA DARAJA YA UBORA HAPA DUNIANI NA KESHO SIKU YA MALIPO.
WITO HUO UMETOLEWA LEO NA UKHTI RAMLA RAMADHANI WAKATI
AKIZUNGUMZA NA WANAWAKE WAKIISLAM KATIKA UKUMBI WA SKULI YA SEKONDARI YA
HAILESALASIE MJINI ZANZIBAR.
AKIZUNGUMZIA MADA KUHUSU KUPENDA MTUME MUHAMMAD S.A.W
AMEBAINISHA KUWA HAKUNA MAANA YAKUMSWALIA PEKEE BALI NI KUTEKELEZA KWA VITENDO
SUNA ZAKE NA KUEPUKA MAKATAZO YAKE.
HATA HIVYO UKHTI RAMLA AMEWATAKA WAISLAM KUDUMISHA
NAKUYAENZI MATUKUFU YA DINI YAO YALIYOBAINISHWA KATIKA QUR-AN KWA KUYAFANYA
KUWA NDIO DIRA YA MAISHA YAO.
MUHADHARA HUO WA WANAWAKE WAKIISLAM UMEHURIWA NA WAISLAM
KUTOKA MJINI NA MAENEO JIRANI.
No comments:
Post a Comment