BAADHI YA VIONGOZI WA DINI NCHINI
TANZANIA WAMEZUNGUMZIA VURUGU ZILIZOFANYWA WIKI ILIYOPITA JIJII DAR ES SALAAM
NA VIJANA WANAOSADIKIKA KUUNDA KUNDI LINALOJULIKANA KAMA PANYA ROAD.
SHEIKH MKUU WA MKOA WA DAR ES SALAAM, ALHADI MUSSA,
AMESEMA KUWA UKOSEFU WA AJIRA NI MOJA YA SABABU ZINAZOZALISHA MAKUNDI YA AJABU, HIVYO SERIKALI INAPASWA KUJIPANGA NA KUTENGENEZA MIFUMO YA AJIRA KWA
VIJANA, ILI KUWAEPUSHA KUJIINGIZA KATIKA MAKUNDI TISHIO NA HATARI.
AMEONGEZA KUWA, VIJANA HAO
WANAVAMIA, KUPORA NA KUUMIZA WATU OVYO, NA KWAMBA UKOSEFU WA AJIRA KWA VIJANA
NI BOMU KUBWA NA BAYA
SANA ZAIDI.
NAYE MCHUNGAJI IFRAHIMU MWANSASU WA KANISA LA
HOSANA LIFE MISSION, AMESEMA KWAMBA MAKUNDI HAYO YA UHALIFU YANASABABISHWA NA MALEZI
MABAYA YA KIIMANI NA KITABIA, KITU ALICHOKIRI KWAMBA HATA
YEYE AMEWAHI KUPITIA AKIWA KIJANA HAPO KABLA,
NA KUITAKA SERIKALI IKAE NAO
NA KUJUA SABABU YA VIJANA HAO KUWA HIVYO.
MWISHONI MWA WIKI ILIYOPITA,
KUNDI LA PANYA ROAD LILIZUA TAFRANI KUBWA JIJINI DAR ES SALAAM, BAADA YA
KUWAVAMIA, KUWAPORA NA KUWAJERUHI WATU KATIKA MAENEO MBALIMBALI YA MJI HUO, LAKINI JESHI LA POLISI CHINI YA KAMANDA SULEIMAN KOVA LILIFANIKIWA KUDHIBITI KUNDI
HILO.
No comments:
Post a Comment