WILAYA NDOGO TUMbATU.
wananchi wa kisiwa cha tumbatu wametakiwa kuendelea
kushikamana katika kufanikisha sherehe za kuzaliwa kwa mtume muhammad (s.a.w) zinazoendeleo
kisiwani humo .
Wito huo umetolewa kwa nyakati tofauti na wakuu wa
kamati za maulidi kisiwani tumbatu wakiwa katika matayarisho ya maulidi
makuu ambayo husomwa kila mwezi huu wa mfunguo sita aliozaliwa
mtume muhammad s.a.w .
Akizungumza na adhana fm mmoja kati ya wanakamati ya
maulidi makuu ya tumbatu jongoe mzee Hassan amesema kuwa maulidi ya tumbatu
ni ya karne nyingi ambapo yamerithiwa kutoka kwa mababu .
Sherehe za kuzaliwa mtume ( swa ) hazina muda maalum
kisiwani tumbatu lakini kwa mwezi huu hufanywa kila siku kwa utaratibu wa
madarasa za qurani zilizopo kisiwani humo na huhitimishwa mwezi 27 mfunguo sita
kaika kijiji cha tumbatu jongoe na mwezi 28 huko tumbatu kichangani .
No comments:
Post a Comment