Zanzibar.
Katibu Mkuu wa chama CHAMA CHA MAPINDUZI Abdulrahman
Kinana amesema KUWA mambo mengi yanayozungumzwa kuhusu baadhi ya wanachama
wanaotajwa kuwania urais hayana ukweli, hakuna atakayefukuzwa uanachama.
Kinana aMEyasema hayo jana mjini ZANZIBAR kuhusu mambo
yaliyojitokeza kwa wagombea wa nafasi za urais kabla ya kufanyika kwa Uchaguzi
Mkuu, Oktoba.
Kamati Kuu ya CCM hadi jana jioni ilikuwa ikiendelea na
kikao chake kwenye ofisi kuu ya chama HICHO, Kisiwandui MJINI Zanzibar.
Kauli ya Kinana imekuja baada ya kuwEpo kwa minong’ono
kuwa baadhi ya makada waliojitokeza kutangaza NA kuonyesha nia kuutaka urais
watachukuliwa hatua, zikiwamo ZAKUFUKUZWA.
Wakati Kinana akijaribu kuwaondoa Khofu vigogo wanaowania
nafasi hiyo, tayari wagombea hao wamepiga kambi mjini ZANZIBAR, baadhi yao
wakiendesha kampeni za chini chini, tOKEA kumalizika kwa sherehe za Mapinduzi.
Wagombea hao wamekuwa wakipishana kuingia visiwani na
kukutana na baadhi ya wajumbe wa Halmshauri Kuu ya CCM na mkutano mkuu kila
upande ukijiimarisha kisiasa kabla ya mchakato wa kumpata mgombea wa urais
kupitia chama hicho Mei mwaka huu.
No comments:
Post a Comment