PEMBA.
MAKAMU WA PILI WA RAIS WA ZANZIBAR BALOZI SEIF ALI IDDI
AMELISHAURI SHIRIKA LA TAIFA BIASHARA
ZANZIBAR { ZSTC } KUANGALIA UWEZEKANO WA KUJENGA KITEGA UCHUMI CHA HOTELI YA
KIMATAIFA NDANI YA ENEO LA KIWANDA CHA MAKONYO WAWI CHAKE CHAKE KISIWANI PEMBA
ILI KUONGEZA MAPATO YAKE.
BALOZI SEIF AMETOA
USHAURI HUO WAKATI AKIUFUNGUA RASMI UKUMBI WA KISASA WA MIKUTANO WA SHIRIKA LA
TAIFA LA BIASHARA ZANZIBAR { ZSTC } {MAKONYO CONFERENCE HALL } KATIKA
KIWANDA CHA MAKONYO WAWI CHAKE CHAKE
IKIWA NI SHAMRA SHAMRA ZA MAADHIMISHO YA KUSHEREHEKEA MIAKA 51 YA
MAPINDUZI YA ZANZIBAR YA MWAKA 1964.
AMESEMA KUWA HATUA
HIYO YA UJENZI WA HOTELI YA KIMATAIFA PIA ITASAIDIA KUONDOKANA NA USUMBUFU WA
MALAZI KWA WAGENI MBALI MBALI WA KITAIFA NA KIMATAIFA WATAKAOFIKA KATIKA UKUMBI
MPYA ULIOJENGWA NA SHIRIKA HILO KWA AJILI YA MIKUTANO.
BALOZI SEIF ALISEMA SHIRIKA LA TAIFA LA BIASHARA ZANZIBAR
NI MIONGONI MWA MASHIRIKA YA UMMA YANAYOFANYA KAZI ZAKE VIZURI
AMBAPO UJENZI WA UKUMBI WAKE WA MIKUTANO WA MAKONYO NI SEHEMU MOJA WAPO
YA MAGEUZI YA MAENDELEO YANAYOENDELEA KUTEKELEZWA NA SHIRIKA HILO.
AMEUPONGEZA UONGOZI NA WATENDAJI WA SHIRIKA LA
TAIFA LA BIASHARA ZANZIBAR KWA JUHUDI ZAO ZINAZOPELEKEA ZAO LA KARAFUU NCHINI
KUZALISHWA KWA WINGI NA KUPATIKANA KWA BEI NZURI YA MAUZO KWA WAKULIMA.
MAPEMA MWENYEKITI WA BODI YA WAKURUGENZI WA SHIRIKA LA
ZSTC BWANA KASSIM MAALIM SULEIMAN ALISEMA KUWA SHIRIKA HILO LIMO KATIKA
HARAKATI ZA MAGEUZI ILIYOJIPANGIA KATIKA KIPINDI CHA MIAKA 10.
AKISOMA RISALA YA WAFANYAKAZI WA SHIRIKA HILO
MWAKILISHI WA CHAMA CHA TUICO – ZSTC NDUGU SULEIMAN JUMA ALISEMA WAFANYAKAZI WA
SHIRIKA HILO WAMEAHIDI KUTEKELEZA WAJIBU WAO KWA NGUVU ZAO ZOTE.
AKIMKARIBISHA MGENI RASMI KATIKA HAFLA HIYO WAZIRI WA
BIASHARA, VIWANDA NA MASOKO ZANZIBAR
NASSOR AHMED MAZRUI ALIWATAKA WANANCHI KUSHIRIKIANA NA UONGOZI NA
WATENDAJI WA SHIRIKA LA ZSTC AMBALO NDILO LINALOJENGA UCHUMI NA MAENDELEO YA
TAIFA.
UKUMBI WA MIKUTANO WA MAKONYO ULIOPO WAWI CHAKE CHAKE
KISIWANI PEMBA UJENZI WAKE UMEGHARIMU
ZAIDI YA SHILINGI ZA KITANZANIA MILIONI MIA NNE NA THAMANINI NA NANE
{ 488,000,000/-.
No comments:
Post a Comment