tangazo

tangazo

Saturday, January 10, 2015

ZAIDI YA SHILINGI MILIONI SABIINI NA TANO LAKI TATU NA ARUBAINI NA TANO ELFU ZIMETUMIKA KATIKA USAMBAZAJI WA MRADI WA UMEME KATIKA KIJIji CHA FUKUCHANI WILAYA YA KASKAZINI “A” UNGUJA.



wilaya ya kskazini a.
ZAIDI YA SHILINGI MILIONI SABIINI NA TANO LAKI TATU NA ARUBAINI NA TANO ELFU ZIMETUMIKA KATIKA  USAMBAZAJI  WA MRADI WA UMEME KATIKA KIJIji CHA FUKUCHANI  WILAYA YA KASKAZINI “A” UNGUJA.
AKIZINDUA MRADI HUO WAZIRI WA ELIMU NA MAFUNZO YA AMALI ZANZIBAR  ALI JUMA SHAMHUNA IKIWA NI SHAMRA SHAMRA ZA KUTIMIA MIAKA 51 YA MAPINDUZI ya zanzibar AMESEMA kuwa SERIKALI YA MAPINDUZI ITAENDELEA KUWAPATIA WANANCHI HUDUMA MUHIMu  ILI WAWEZE KUNUFAIKA NA MATUNDA YA MAPINDUZI YA MWAKA 1964.
AMESEMA KUWA WANANCHI WANAHAKI YA KUUNGA NISHATI HIYO  KWA   KUFUATA TARATIBU ZA KISHERIA  KWA  LENGO KUJINUFAISHA NA KUJIKWAMUA NA HALI YA KIUCHUMi.
KWA  UPANDE WAKE NAIBU KATIBU MKUU WIZARA YA MAJI MAAKAZI NA NISHATI MUSTAFA ABUOD JUMBE AMESEMA    kuwa MOJA YA SERA YA SERIKALI YA MAPINDUZI NI KUHAKIKISHA KUWA HUDUMA MUHIMU ZA KIJAMII IKIWEMO UMEME ZINAWAFIKIA WANACHI BILA YA USUMBUFU.
AMEFAHAMISHA KUWA USAMbAZAJI WA HUDUMA HIYO KATIKA KIJIJI CHA FUKUCHANI uMEHUSISHA UWEKAJI WA TRANSFOMA MOJA NA UJENZI WA LAINI NDOGO ZA UMEME yENYE UREFU WA KILOMITA MBILI  ILI IWEZE KUWANUFAISHA NA WAKAAZI WA ViJIJI VYA JIRANI.
SAMBA NA HAYO AMEWATAKA WANANCHI WA FUKUCHANI KUKULINDA MIUNDO MBINI HIYO NA KUEPUKA TABIA KUCHOMA  MOTO KATIKA VYANZO VYA MIUNDOMBINU HIYO.

No comments:

Post a Comment