tangazo

tangazo

Wednesday, February 25, 2015

SERIKALI YA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA IMEIAGIZATUME YA HAKI ZA BINADAMU NA UTAWALA BORA KUIBUA MASUALA YANAYOATHIRI UZINGATIAJI WA HAKI ZA BINADAMU ILI HATUA STAHIKI ZICHUKULIWE NA HIVYO KUIMARISHA MISINGI YA HAKI NA UTAWALA BORA NCHINI.



DAR-ES-SALAAM.

SERIKALI YA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA IMEIAGIZATUME YA HAKI ZA BINADAMU NA UTAWALA BORA KUIBUA MASUALA YANAYOATHIRI UZINGATIAJI WA HAKI ZA BINADAMU ILI HATUA STAHIKI ZICHUKULIWE NA HIVYO KUIMARISHA MISINGI YA HAKI NA UTAWALA BORA NCHINI.

AKIZUNGUMZA NA VIONGOZI WA TUME HIYO MJINI DAR ES SALAAM, WAZIRI WA KATIBA NA SHERIA DKT. ASHA–ROSE MIGIRO AMESEMA KUWA SERIKALI INA WAJIBU WA KUZINGATIA HAKI ZA BINADAMU KATIKA UTEKELEZAJI WA MAJUKUMU YAKE.

TUME YA HAKI ZA BINADAMU NA UTAWALA BORA ILIANZISHWA MWAKA 2000 NA KUANZA KAZI RASMI MWAKA 2002 ILI, KUTOA USHAURI KWA SERIKALI NA VYOMBO VINGINE VYA UMMA NA VYA SEKTA BINAFSI KUHUSU HAKI ZA BINADAMU NA UTAWALA BORA.

AKIZUNGUMZA KATIKA MKUTANO HUO, NAIBU WAZIRI WA WIZARAHIYO UMMY MWALIMU AMESEMA KUWA NI MUHIMU KWA TUME HIYO KUONGEZA KASI YA KUTOA ELIMU KWA UMMA KUHUSU UZINGATIAJI WA HAKI ZA BINADAMU NA UTAWALA BORA KWA KUTUMIA TEKNOLOJIA YA KHABARI NA MAWASILIANO ILI KUWAFIKIA WANANCHI WENGI KWA KASI NA HARAKA.

WARIOBA AMEVITAKA VYAMA VYA SIASA NCHINI HUMO KUZINGATIA MATAKWA YA WANANCHI KATIKA SUALA LA KURA YA MAONI



DAR-ES-SALAAM.

ALIYEKUWA MWENYEKITI WA TUME YA MABADILIKO YA KATIBA, JAJI MKUU MSTAAFU JOSEPH SINDE WARIOBA AMEVITAKA VYAMA VYA SIASA NCHINI HUMO KUZINGATIA MATAKWA YA WANANCHI KATIKA SUALA  LA KURA YA MAONI YA KATIBA INAYOPENDEKEZWA BADALA YA KUWAGAWA.

WARIOBA AMESEMA  KUWA ANAAMINI KWAMBA, BAADHI YA VIPENGELE VILIVYOKATALIWA KATIKA RASIMU YA KATIBA, IPO SIKU VITAFANYIWA KAZI ILI KUONDOA MIGONGANO HUKU AKISISITIZA, KISHERIA KURA YA MAONI SIYO MWISHO WA MCHAKATO.

WAZIRI MKUU HUYO MSTAAFU WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA AMESEMA KUWA, KWA SASA, BADALA YA KUWAWEKA WANANCHI PAMOJA NA KUKUBALIANA WANACHOTAKA , UPO MVUTANO HUKU WENGINE WAKITAKA KATIBA ILIYOPENDEKEZWA IKUBALIWE NA WENGINE WAKITAKA WANANCHI WAIKATAE.

HAYO YAMEKUJA HUKU KAMBI YA UPINZANI NCHINI KUPITIA UMOJA WA KATIBA YA WANANCHI (UKAWA) UKITANGAZA KUTOSHIRIKI KATIKA KURA IJAYO YA MAONI YA KATIBA.

Monday, February 23, 2015

JAMII YAASWA KUWASAIDIA VIJANA JUU YA MADAWA YA KULEVYA



JAMII  NCHINI IMETAKIWA KUJENGA UMOJA NA MASHIRIKIANO KWA LENGO LA KUTIMIZA WAJIBU KATIKA KUPAMBANA NA MADAWA YAKULEVYA ILI KUJENGA TAIFA JEMA KWA MASLAHI YA NCHI.

AKIZUNGUMZA NA NA ADHANA FM MWENYE KITI WA RECOVER RECOMMUNITY SLEMANI  MOHD MAULID AMESEMA  KUWA ILI VIJANA KUWACHA MADAWA YA KULEVYA  NI LAZIMA  JAMII KUSHIRIKIANA  KATIKA  KUPAMBANA NA MADAWA YA KULEVYA. 

AMEELEZA KUWA WAO KAMA SOBER  HOUSE WAMEKUWA WAKIWASAIDIAVIJANA  KWA JUHUDI KUBWA  LAKINI KUMEKUWA NA WATU AMBAO WASIOKUWA NA UCHUNGU WA VIJANA NA TAIFA KWA UJUMLA HUWAHARIBU VIJANA NA KUDUMAZA HUDUMA ZA MAENDELEO KATIKA NCHI.

AMESEMA  KUWA HIVI SASA UHALIFU UMEZIDI KUTOKANA  NA VIJANA WENGI KUINGIA KWENYE BADAWA YA KULEVYA NA KUSABABISHA  UHALIFU  KWA JAMII HIVYO  INATAKIWA KUPANGA MIKAKTI KATIKA VIWANJA VYA NDEGE ,BANDARI  NA NJIA NYENGINE ILI KUPUNGUZA UINGIZWAJI WA MADAWA HAYO.

KUNA ULAZIMU WA VIJANA KUJUA WAASISI WAO



ZANZIBAR.

MAKAMU WA PILI WA RAIS WA ZANZIBAR BALOZI SEIF ALI AMESEMA KUWA  KIZAZI KIPYA KINAPASWA KUFAHAMU  AZMA YA WAASISI WA TAIFA LA TANZANIA  MAREHEMU MZEE ABEID AMANI KARUME NA BABA WA TAIFA MWALIMU JULIUS KAMBARAGE NYERERE WAKATI WALIPOKUWA MSTARI WA MBELE KUDAI UHURU NA HAKI ZA JAMII YA WATU WOTE.
BALOZI SEIF AMEYASEMA HAYO WAKATI AKIZUNGUMZA NA WAJUMBE WA BODI YA UDHAMINI WA MFUKO WA KUWAENZI WAASISI WA TAIFA LA TANZANIA ULIOONGOZWA NA MWENYEKITI WAKE KANAL MSTAAFU KABENGA NSA KAISI ALIOKUTANA NAO OFISINI KWAKE    VUGA MJINI ZANZIBAR.
ALISEMA WATOTO WALIOWENGI WA  KIZAZI KIPYA BADO WANAENDELEA KUWA NJIA PANDA WAKIKOSA KUMBU KUMBU KADHAA ZA VIONGOZI WAASISI AMBAZO ZINGEWAPA FURSA NA NAFASI PANA YA KUELEWA MALENGO SAHIHI YA WAASISI HAO.
AMESEMA KUWA KUNA  MATAIFA MENGI DUNIANI KAMA VIETNAM, JAMUHURI YA WATU WA CHINA NA KOREA YA KASKAZINI YENYE HISTORIA KUBWA YA KUENZI KAZI NA KUMBU KUMBU ZA WAASISI WAO KITENDO AMBACHO BODI HIYO ITASTAHIKI KUIGA MFANO HUO.
MAPEMA MWENYEKITI WA BODI HIYO KANAL MSTAAFU KABENGA NSA KAISI AMESEMA KUWA JUKUMU KUBWA LA BODI HIYO NI KUKUSANYA KUMBU KUMBU ZA WAASISI TAIFA LA TANZANIA NA KUZIHIFADHI KWA FAIDA YA VIZAZI VIPYA.
KANAL MSTAAFU KABENGA AMESEMA  KUWA BODI HIYO TAYARI IMESHAANDAA MIKAKATI YA JINSI YA KUPATA UWEZO WA KIFEDHA ZITAKAZOKIDHI UANZISHWAJI WA VITUO VIWILI VYA KUMBU KUMBU VITAKAVYOWEKWA TANZANIA BARA NA ZANZIBAR.

WATU 1000 WALIZUNGUKA SINAGOGI



oslo.
Zaidi ya watu 1000 wengi wao wakiwa waislamu wameunda mviringo na kulizunguka sinagogi nchini Norway, kuonyesha umoja wao kufuatia mashambulizi kadhaa yaliyowalenga wayahudi barani Ulaya.
Wakati waumini wa kiyahudi walipokuwa wakitoka ndani ya sinagogi katika mji mkuu wa Norway Oslo, kulikuwa na shangwe wakati vijana wa kiislamu walipowazingira kama ishara ya amani.
Warsha hiyo ilipangwa na vijana wa kiislamu na kufanyika wiki chache baada ya kijana mmoja mzaliwa wa Denmark mwenye asili ya Kiphalestina kuwaua watu wawili .