DAR-ES-SALAAM.
ALIYEKUWA MWENYEKITI WA TUME YA
MABADILIKO YA KATIBA, JAJI MKUU MSTAAFU JOSEPH SINDE WARIOBA AMEVITAKA VYAMA
VYA SIASA NCHINI HUMO KUZINGATIA MATAKWA YA WANANCHI KATIKA SUALA LA KURA YA MAONI YA KATIBA INAYOPENDEKEZWA
BADALA YA KUWAGAWA.
WARIOBA AMESEMA KUWA ANAAMINI KWAMBA, BAADHI YA VIPENGELE
VILIVYOKATALIWA KATIKA RASIMU YA KATIBA, IPO SIKU VITAFANYIWA KAZI ILI KUONDOA
MIGONGANO HUKU AKISISITIZA, KISHERIA KURA YA MAONI SIYO MWISHO WA MCHAKATO.
WAZIRI MKUU HUYO MSTAAFU WA JAMHURI
YA MUUNGANO WA TANZANIA AMESEMA KUWA, KWA SASA, BADALA YA KUWAWEKA WANANCHI
PAMOJA NA KUKUBALIANA WANACHOTAKA , UPO MVUTANO HUKU WENGINE WAKITAKA KATIBA
ILIYOPENDEKEZWA IKUBALIWE NA WENGINE WAKITAKA WANANCHI WAIKATAE.
HAYO YAMEKUJA HUKU KAMBI YA UPINZANI
NCHINI KUPITIA UMOJA WA KATIBA YA WANANCHI (UKAWA) UKITANGAZA KUTOSHIRIKI
KATIKA KURA IJAYO YA MAONI YA KATIBA.
No comments:
Post a Comment