Waziri Mkuu wa Serikali ya Jamuhuri ya Muungano
wa Tanzania Mizengo Peter Pinda
aMEwapongeza wanamichezo wa Timu za Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
kwa kuliletea sifa kubwa Bunge hilo kATIKA mashindano ya michezo mbali mbali ya
Kitaifa na Kimataifa.
Pinda aMEtoa pongezi hizo katika Tafrija maalum
ya kuukaribisha mwaka mpya zilizofanyika katika majengo ya Bunge la Jamhuri YA
MUUNGANO WA TANZANIA Mjini DodomaKATIKA
hafla iliyokwenda sambamba na kuwapongeza wanamichezo wa Bunge hilo
baada ya kushinda michezo MBALI MBALI
katika mashindano ya Mabunge ya Jumuiya ya Afrika Mashariki yaliyofanyika Mjini
Arusha Tanzania.
aMEsema kUWA michezo inatoa nafasi kubwa ya
ushirikiano ambayo ni kielelezo cha msingi kinacHOLETA Viongozi bora
wanaotokana na sekta ya michezo.
AMEishauri Kamati ya Uongozi wa Michezo ya
Bunge hilo kufikiria umuhimu wa kuwashirikisha wawakilishi wa wanamichezo wa
mabunge wanachama kwenye tafrija kama hizo kwa lengo la kusherehekea nao pamoja
ili kudumisha ushirikiano pamoja na ujirani mwema.
Mapema Mwenyekiti wa Bunge Sports Club Iddi
Azan aMEsema KUWA ongezeko la michezo
mbali mbali kwenye mashindano ya Timu za Mabunge ya Afrika ya Mashariki
linatokana na azimio la Mabunge ya Jumuiya hiyo la kuzitaka Nchi Wanachama
kuongeza michezo mengine kwenye mashindano hayo.
Mwenyekiti HUYO aMESEMA KUWA mAshindano ya Mabunge hayo yalikuwa
yakishirikisha michezo miwili tuu
Kandanda na Pete ambapo kwa sasa ipo riadha, mbio za vijiti, kuvuta
kamba, kufukuza kuku ikiwemo pia ile ya watu wenye mahitaji maalum { Walemavu
}.
Mwenyekiti huyo wa Bunge Sports Club alielezea
faraja yake kutokana na ushiriki mzuri wa wanamichezo wa Timu za Bunge la
Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania kwenye mashindano mbali mbali ya Mabunge na
kuleta ushindi katika michezo tofauti.
No comments:
Post a Comment