Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim
Seif Sharif Hamad, amewasili mjini Dubai UMOJA WA FALME ZAKIARABU kwa ajili ya
kuanza ziara rasmi ya kiserikali nchini Qatar.
Mhe. Maalim Seif amewasili mjini Dubai jana
mchana akitokea nchini India ambako alikwenda kwa ajili ya kufanya uchunguzi wa
kawaida wa afya yake.
Katika ziara hiyo ya siku nne nchini Qatar,
Maalim Seif ataambatana na ujumbe wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar akiwemo
katibu mkuu ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais Dkt. Omar Dadi Shajak.
No comments:
Post a Comment