PEMBA.
JESHI
LA POLISI MKOA WA KUSINI PEMBA, LINAWASHIKILIA WATU WAWILI KWA TUHUMA ZA MAUAJI
YA MAKAME ALI SULEIMAN (DUDE), ALIYEUAWA KATIKA MAZINGIRA YA KUTATANISHA.
AKIZUNGUMZA
NA MWANDISHI WA HABARI HIZI, KAMANDA WA POLISI MKOA HUO, JUMA YUSSUF ALI,
ALISEMA MAREHEMU ALIOKOTWA CHINI YA MNAZI AMBAO UNAGEMWA POMBE, HALI
INAYOONESHA KULIKUWEPO UGOMVI WA KUWANIA POMBE BAINA YA MAREHEMU NA WATU WALIOFANYA
MAUAJI HAYO.
ALISEMA
BAADA YA UPELELEZI KUKAMILIKA, WATUHUMIWA WATAFIKISHWA KATIKA VYOMBO VYA SHERIA
ILI SHERIA ICHUKUE MKONDO WAKE.
TUKIO
HILO LILILOTOKEA USIKU WA KUAMKIA FEBUARI 6 KATIKA BONDE LA OKA KANGANI WILAYA
YA MKOANI, BAADA YA WANANCHI WALIOKUWA WAKIPITA NJIANI KUONA MWILI WA MAREHEMU
UKIWA UMETELEKEZWA.
MAREHEMU
ALIKATWA BEGA LA KUSHOTO NA KUTOLEWA LOTE, KUHARIBIWA SEHEMU ZA USONI NA MACHO,
KUPASULIWA KICHWANI, KUKATWA MASIKIO NA KUKATWA VIDOLE.
AIDHA
ALISEMA MTU MMOJA ANASHIKILIWA BAADA YA KUVAMIA NYUMBA MOJA KATIKA KIJIJI CHA
PUJINI NA TAYARI AMESHAFIKISHWA MAHAKAMANI.
KAMANDA
HUYO ALIMTAJA MTUHUMIWA HUYO KWA JINA MOJA LA FESHA, AMBAYE ANA REKODI NYINGI
ZA MATUKIO YA UHALIFU.
No comments:
Post a Comment