ZANZIBAR.
MAKAMU WA PILI WA RAIS WA ZANZIBAR BALOZI SEIF ALI
AMESEMA KUWA KIZAZI KIPYA KINAPASWA
KUFAHAMU AZMA YA WAASISI WA TAIFA LA TANZANIA MAREHEMU MZEE ABEID
AMANI KARUME NA BABA WA TAIFA MWALIMU JULIUS KAMBARAGE NYERERE WAKATI WALIPOKUWA
MSTARI WA MBELE KUDAI UHURU NA HAKI ZA JAMII YA WATU WOTE.
BALOZI SEIF AMEYASEMA HAYO WAKATI AKIZUNGUMZA NA WAJUMBE
WA BODI YA UDHAMINI WA MFUKO WA KUWAENZI WAASISI WA TAIFA LA TANZANIA
ULIOONGOZWA NA MWENYEKITI WAKE KANAL MSTAAFU KABENGA NSA KAISI ALIOKUTANA NAO
OFISINI KWAKE VUGA MJINI ZANZIBAR.
ALISEMA WATOTO WALIOWENGI WA KIZAZI KIPYA BADO
WANAENDELEA KUWA NJIA PANDA WAKIKOSA KUMBU KUMBU KADHAA ZA VIONGOZI WAASISI
AMBAZO ZINGEWAPA FURSA NA NAFASI PANA YA KUELEWA MALENGO SAHIHI YA WAASISI HAO.
AMESEMA KUWA KUNA
MATAIFA MENGI DUNIANI KAMA VIETNAM, JAMUHURI YA WATU WA CHINA NA KOREA
YA KASKAZINI YENYE HISTORIA KUBWA YA KUENZI KAZI NA KUMBU KUMBU ZA WAASISI WAO
KITENDO AMBACHO BODI HIYO ITASTAHIKI KUIGA MFANO HUO.
MAPEMA MWENYEKITI WA BODI HIYO KANAL MSTAAFU KABENGA NSA
KAISI AMESEMA KUWA JUKUMU KUBWA LA BODI HIYO NI KUKUSANYA KUMBU KUMBU ZA
WAASISI TAIFA LA TANZANIA NA KUZIHIFADHI KWA FAIDA YA VIZAZI VIPYA.
KANAL MSTAAFU KABENGA AMESEMA KUWA BODI HIYO TAYARI IMESHAANDAA MIKAKATI YA
JINSI YA KUPATA UWEZO WA KIFEDHA ZITAKAZOKIDHI UANZISHWAJI WA VITUO VIWILI VYA
KUMBU KUMBU VITAKAVYOWEKWA TANZANIA BARA NA ZANZIBAR.
No comments:
Post a Comment