ZANZIBAR.
RAIS wa Zanzibar Dk. Ali Mohamed Shein amesisitiza haja ya kuwatumia
wataalamu wazalendo katika kazi za kitaalamu za Serikali.
Dk. Shein aMEyasema hayo leo katika mkutano kati yake
na Uongozi wa Ofisi ya Rais na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Ikulu mjini
Zanzibar, AMBAO ULIKUWA lengo la
kuangalia Utekelezaji wa Malengo ya Mpango Kazi wa Ofisi hiyo hiyo kwa robo
mbili kati ya Julai hadi Disemba 2014.
Katika maelezo yake Dk. Shein, alipongeza hatua
zilizochukuliwa na Ofisi hiyo katika kuhakikisha malengo yaliwekwa yanafikiwa
pamoja na kutekelezwa kwa ufanisi mkubwa.
Aidha, Dk. Shein alitumia fursa hiyo, kuusisitiza
uongozi wa Wizara hiyo akiwemo Waziri na Katibu Mkuu wake kuendelea na
utaratibu uliwekwa na Serikali wa kutoa taarifa kwa wananchi kwa muda
uliopangwa kupitia vyombo vya habari ili kuwaeleza mafanikio yaliopatika.
Dk. Shein alisema kuwa Serikali ya Mapinduzi ya
Zanzibar imefanya mambo mengi na kupata mafanikio makubwa ambayo inapaswa
wananchi kupewa taarifa juu ya mambo hayo sambamba na kuelezwa changamoto
zilizopo na jinsi juhudi zinazochukuliwa na Serikali katika kuzitafutia
ufumbuzi.
Sambamba na hayo, Dk. Shein alieleza juhudi
zinazoendelea kuchukuliwa katika kuimarisha na kuendeleza huduma za kijamii na
miradi ya maendeleo ikiwemo sekta ya maji ambayo licha ya changamoto zilizopo
lakini huduma hiyo imeweza kuimarika kwa kiasi kikubwa hapa nchini.
Mapema akitoa taarifa ya Utekelezaji wa Malengo ya
Mpango Kazi wa Bajeti ya Ofisi hiyo, Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Ikulu na
Utawala Bora Dk. Mwinyihaji Makame alieleza majukumu, malengo, mafanikio na
changamoto zilizopo na juhudi zinzochukuliwa kuzitafutia ufumbuzi changamoto
hizo ndani ya Idara za Ofisi hiyo.
Katika kuhakikisha kuwa matumizi ya rasilimali za
umma yanafanyika kwa kuzingatia uwazi na uwajibikaji Dk. Mwinyihaji alisema
kuwa Ofisi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali Zanzibar
imekamilisha Ukaguzi wa Hesabu katika Wizara na Mashirika ya Serikali.
No comments:
Post a Comment