DAR-ES-SALAAM.
TUME
YA TAIFA YA UCHAGUZI (NEC) IMEPELEKA MBELE TAREHE YA KUANZA KUANDIKISHA WAPIGA
KURA KATIKA DAFTARI LA KUDUMU LA WAPIGA KURA.
ZOEZI HILO LILILOTARAJIWA KUANZA FEBRUARI 19 MWAKA HUU SASA LITAANZA KUFANYIKA
FEBRUARI 23 KATIKA MKOA WA NJOMBE.
AKIZUNGUMZA MJINI DAR ES SALAAM,
MWENYEKITI WA TUME HIYO, JAJI MSTAAFU, DAMIAN LUBUVA, AMESEMA KUWA SABABU YA
KUSOGEZWA MBELE NI KUCHELEWA KUFIKA VIFAA VYA KUANDIKISHA.
AMESEMA KUWA VIFAA VILIVYOPO KWA SASA NI
250 PEKEE AMBAVYO VILITUMIKA KATIKA UANDIKISHAJI WA MAJIRIBIO NA VIFAA VYENGINE
7750, VINASUBIRIWA KUFIKA NCHINI HIVI KARIBUNI.
AIDHA AMESEMA KUWA SABABU NYENGINE YA
KUAKHIRISHWA NI KUITIKIA WITO WA WADAU HASUSAN VYAMA VYA SIASA VILIVYOOMBA
ZOEZI HILO LIPELEKWE MBELE ILI KUPATA MUDA WA KUJIANDAA.
UANDIKISHAJI WA WAPIGA KURA WAPYA
UTAFANYWA KWA KUTUMIA TEKNOLOJIA MPYA YA BIOMETRIC VOTE REGSTRATION ( BVR).
MFUMO HUO MPYA NI WA KUCHUKUA AU KUPIMA
TAARIFA ZA MTU ZA KIBAIOLOJIA AU TABIA YA MWANADAMU NA KUHIFADHI KATIKA KANZI
DATA KWA AJILI YA UTAMBUZI.
No comments:
Post a Comment