ZANZIBAR.
MAKAMO WA PILI WA RAIS WA ZANZIBAR BALOZI SEIF ALI IDDI AMEUAGIZA UONGOZI
WA HALMASHAURI YA WILAYA YA MAGHARIBI PAMOJA NA TAASISI ZINAZOSIMAMIA MASUALA
YA UJENZI KUHAKIKISHA KWAMBA NYUMBA ZILIZOJENGWA NA ZINAZOENDELEA
KUJENGWA KATIKA VIANZIO VYA MAJI VYA DOLE ZINAVUNJWA HARAKA IWEZEKANAVYO.
BALOZI SEIF AMETOA AGIZO HILO WAKATI ALIPOFANYA ZIARA FUPI YA KUKAGUA ENEO
LA MSITU WA KIMAUMBILE LILIOPO MASINGINI DOLE PAMOJA NA LILE YA VIANZIO VYA
MAJI DOLE LINALOONEKANA KUANZA KUVAMIWA KWA UJENZI WA NYUMBA LICHA YA AMRI
ILIYOWAHI KUTOLEWA NA MAMLAKA YA MAJI ZANZIBAR { ZAWA } YA KUZUIA UJENZI HUO.
AMESEMA KUWA HATUA HIYO YA SERIKALI
IMEKUJA KUZINGATIA UHARIBIFU UNAOONEKANA KUENDELEA KUFANYWA KATIKA
VIANZIO VYA MAJI JAMBO AMBALO NI HATARI KWA UCHAFUZI WA MAZINGIRA SAMBAMBA NA AFYA
ZA WANANCHI.
AMESEMA KUWA UONGOZI WA HALMASHAURI HIYO LAZIMA UFANYE UTARATIBU WA
KUWAHAMISHA WATU WOTE WALIOJENGA KATIKA VIANZIO HIVYO VYA MAJI ILI KUENDELEA
KUHESHIMU IPASAVYO MAENEO HAYO MUHIMU KWA USTAWI WA JAMII.
MAKAMU WA PILI WA RAIS WA ZANZIBAR ALIELEZA KWAMBA WATAALAMU WA KILIMO NA
MAZINGIRA WANARUHUSU MAENEO YA VIANZIO VYA MAJI KUTUMIKA KWA KILIMO CHA AINA
MBALI MBALI KUTOKANA NA KUTOCHAFUA NAKUHATARISHA MAZINGIRA YA VIANZIO
HIVYO.
MAPEMA SHEHA WA SHEHIA YA DOLE BWANA IBRAHIM SHAABAN OTHMAN ALIMUELEZA
MAKAMU WA PILI WA RAIS WA ZANZIBAR KWAMBA MAMLAKA YA MAJI ZANZIBAR { ZAWA }
ILIWAHI KUWEKA MABANGO YA MATANGAZO KUJARIBU KUSIMAMISHA UJENZI WA
AINA YOYOTE KWENYE ENEO HILO.
HATA HIVYO SHEHA IBRAHIMU AMESEMA KUWA HARAKATI ZA UJENZI WA NYUMBA
HIZO ZILIZOPO MITA CHACHE KUTOKA KWENYE KISIMA HICHO CHA DOLE ZILIENDELEA
HUKU NYENGINE ZIKIWA KATIKA HATUA YA KUKAMILIKA.
No comments:
Post a Comment