SERIKALI YA MAPINDUZI YA ZANZIBAR IMEELEZA AZMA YAKE
YA KUENDELEA KUIMARISHA UHUSIANO NA USHIRIKIANO WA KIHISTORIA KATI YAKE NA
JAMHURI YA KIISLAMU YA IRAN AMBAYO INAIUNGA MKONO ZANZIBAR KATIKA KUIMARISHA
SEKTA MBALI MBALI ZA MAENDELEO.
RAIS
WA ZANZIBAR NA DK. ALI MOHAMED SHEIN
AMEYASEMA HAYO WAKATI AKIZUNGUMZA NA
WAZIRI WA MAMBO YA NJE WA JAMHURI YA KIISLAMU YA IRAN, JAVAD
ZARIF, IKULU MJINI ZANZIBAR.
KATIKA
MAZUNGUMZO HAYO, DK. SHEIN
AMESEMA KUWA ZANZIBAR INA MENGI YA KUJIFUNZA KUTOKA KWA NDUGU ZAO WA IRAN NA
KUTOA PONGEZI KWA NCHI HIYO KWA KUENDELEA KUIUNGA MKONO ZANZIBAR KATIKA
SEKTA ZA MAENDELEO IKIWEMO SEKTA YA ELIMU NA AFYA.
DK.
SHEIN ALIELEZA KUWA ZANZIBAR
INATHAMINI UHUSIANO NA USHIRIKIANO WA KIHISTORIA KATI YA NCHI MBILI HIZO NA KUSISITIZA
KUWA NCHI HIYO IMEKUWA IKITOA USHIRIKIANO MKUBWA KATIKA SEKTA YA ELIMU KWA
KUTOA NAFASI ZA MAFUNZO KWA VIJANA WA ZANZIBAR KWENDA KUSOMA NCHINI HUMO.
AMESEMA
KUWA ZANZIBAR IMEKUWA NA MABADILIKO MAKUBWA YA KIMAENDELEO HIVYO KUIMARISHWA
KWA UHUSIANO KATI YAKE NA IRAN KUTAZIDI KUKUZA MAENDELEO HAYO
HASUSAN KATIKA SEKTA YA KILIMO MAFUNZO
YA UFUNDI NA AFYA AMBAPO IRAN IMEAHIDI KUIUNGA MKONO ZANZIBAR.
NAE
WAZIRI WA MAMBO YA NJE WA JAMHURI YA KIISLAMU YA IRAN, JAVAD
ZARIF ALIUPONGEZA UHUSIANO NA
USHIRIKIANO WA KIHISTORIA ULIOPO KATI YA NCHI HIYO NA ZANZIBAR NA KUSISITIZA
KUWA ZIARA YAKE NI MIONGONI MWA HATUA ZA KUKUZA UHUSIANO HUO.
WAZIRI
ZARIF ALIMUELEZA DK. SHEIN
KUWA IRAN ITAENDELEA KUIUNGA MKONO ZANZIBAR KATIKA KUIMARISHA SEKTA ZA
MAENDELEO ZIKIWEMO ELIMU, AFYA, UVUVI NA
KILIMO HUKU AKISISITIZA HAJA YA KUKUZA MAHUSIANO KATI YA WIZARA YA
KILIMO YA ZANZIBAR NA ILE YA IRAN KWA LENGO LA KUINUA SEKTA HIYO KWA PANDE ZOTE
MBILI.
No comments:
Post a Comment