SHIMO LA KIZA
SEHEMU YA TATU
sikuambiwa nipeleke vitu kama walivyo wazanzibar na waislam wa zama hizi kutaka gharma kubwa kwa kutaja fanicha mm niliambiwa nipeleke kiasi cha pesa na harusi ikapangwa nakumbuka ilipangwa tarehe sita mwezi wa tisa mwaka 2013 saa kumi jioni
endelea kukiwa na mipango ya harusi ikiendelea mara siku ikafika na majira ya saa tisa na nusu tukaondoka tomondo kuelekea upenja kwa ajili ya ndoa mashallah watu walikuwa wengi kutoka kila kona bagamoyo,Pemba... na miji yote ya unguja lakini hili halikunipa tabu labda kutokana na umarufu wangu katika utumishi wa umma kupitia redio adhana msururu mkubwa wa magari ukiongozwa na watuma salam wa redio adhana na mashekhe na ahlumasjid wa masjid muhusinina tomondo ambao na wao hawakuwa nyuma kuniunga mkono katika jambo langu jema nakumbuka sala ya alasiri mimi na msafara wangu tulisalimchangani shamba majira kama ya saa kumi na nusu tukaingia upenja tukapokelewa kwa bashasha na katika chuo cha kichungwani upenja branchi ndipo nilipokunja goti na mara baada ya kuchukuliwa idhni ya muolewaji shekhe akarudi na na masharti yote ya ndoa yalipotimia ndoa ikafungwa rasmi shamrashamra za hapa na pale hazikukosekana na ikafika muda wa kwenda kumuona mke wangu ukafika taratibu za kidini zikafatwa na mara baada ya hapo nikachukua mke wangu na kurudi nae kwangu miembeni maisha yakaanza kama ilivyo kawaida ya mila na dasturi ya watu wa pwani chai za hapa na pale zikawa za pishana nilikuwa madhubuti sana katika misingi ya dini yangu sikuwa tayari kuruhusu upumbavu katika ndoa yangu kama ilivyokawaida asona wivu dayuthi na dayuthi haingii peponi na pepo naipenda na naitamani kuingia nilizidi kumuomba allah aniwafikishe kwenye kheri masikini we kwa vile sina elimu ya ghaibu wiki tatu ya ndoa yangu ikaingia dosari ..........................................nini kiliendelea ungana nami katika sehemu ya nne katika simulizi hii ya kweli katika maisha yangu mm binafsi
uislam ndio liwazo langu
No comments:
Post a Comment