ZANZIBAR.
Vikosi vya ulinzi
na Uokozi kwa kushirikiana na wafanyakazi wa Wizara ya Kilimo na Mali
Asili na wananchi wa Mkoa wa Kusini Unguja wamefanikiwa kuuzima moto katika
Hifadhi ya Taifa ya Msitu wa Jozani ulioibuka upande wa magharibi ya
msitu huo maarufu Jozani Kovu.
Makamu wa Pili wa Rais
wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi alifika KATIKA eneo la tukio kuangalia athari
iliyotokea kwenye msitu huo wenye hadhi ya Kimataifa kutokana na mazingira yake
ya miti pamoja na wanyama adimu Duniani.
Hekta 17 kati ya
elfu 5,000 zilizomo ndani ya Hifadhi ya Taifa ya Msitu huo
zimeathirika kwa moto unaodhaniwa kuibuka juzi jioni
kutokana na wavunaji haramu wa Asali.
Katibu Mkuu Wizara ya
Kilimo na Mali Asili Zanzibar Nd. Afan Othman Maalim alimueleza Balozi Seif
kwamba juhudi za vikosi vya ulinzi kwa kushirikiana na wananchi wa Vijiji
Jirani imesaidia kuudhibiti moto huo usiingie kwenye msitu mkubwa.
HATA HIVYO KIONGOZI
HUYO AMEBAINISHA KUWA kuathirika kwa
msitu huo LICHA YAkuchafuka kwa mazingira katika eneo hilo la hifadhi ya
Taifa NA kilimo cha mpunga katika Bonde la
Cheju kinaweza kuwa hatarini kutoweka kwa kukosa rasilmali ya maji.
Akitoa shukrani Makamu
wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi ameiagiza Wizara ya Kilimo kwa
kushirikiana na uongozi wa Serikali ya Mkoa wa Kusini Unguja kuchukuwa hatua za
kukabiliana na wagemaji haramu wa asali ili kujaribu kuzuia uharibifu wa
mazingira.
Balozi Seif alisema kwa
niaba yake na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar amevipongeza Vikosi vya ulinzi
kwa kushirikiana na wananchi kutokana na juhudi kubwa walizochukuwa
za kufanikiwa kuuzima moto huo.
AMEfahamisha kUWA
Jozani ikiwa ni miongoni mwa Misitu miwili mikubwa katika Visiwa vya
Zanzibar UkiweMo na wa Ngezi Kisiwani Pemba lazima iendelee
kudhibitiwa kwa nguvu zote.
No comments:
Post a Comment