DAR-ES-SALAAM.
TANZANIA ITAKUWA MWENYEJI WA MKUTANO WA 22 WA KIMATAIFA WA CHAMA CHA
WAHASIBU WAKUU WA SERIKALI WA NCHI ZA MASHARIKI NA KUSINI MWA AFRIKA
UTAKAOFANYIKA NCHINI KUANZIA MACHI 09, HADI 12 MWAKA 2015.
KAULI HIYO IMETOLEWA NA MHASIBU MKUU WA SERIKALI,MWANAIDI MTANDA KWA
NIABA YA KATIBU MKUU WA WIZARA YA FEDHA DKT. SERVACIUS LIKWELILE MJINI DAR ES SALAAM ALIPOKUWA AKIZUNGUMZA NA
WAANDISHI WA KHABARI KUHUSIANA NA MKUTANO HUO UTAKAOFANYIKA NCHINI.
MHASIBU HUYO AMESEMA KUWA MGENI
RASMI KATIKA MKUTANO HUO ANATARAJIWA KUWA RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA
TANZANIA DKT. JAKAYA KIKWETE.
KATIKA MKUTANO HUO, MADA MBALIMBALI ZINATARAJIWA KUJADILIWA ZIKILENGA
KUKUZA USHIRIKIANO MIONGONI MWA NCHI WANACHAMA KATIKA MASUALA YA HESABU ZA
SERIKALI NA KUTOA FURSA YA KUWA NA JUKWAA KWA AJILI YA WASHIRIKI ILI KUFANYA
TATHMINI KWA KUJADILIANA NA KUBADILISHANA UZOEFU MBALI MBALI.
AIDHA, MKUTANO HUO UNALENGA KUHAMASISHA MAENDELEO YA WATENDAJI WAHASIBU
WA SERIKALI NA KUTOA MAFUNZO STAHIKI KUPITIA UTEKELEZAJI WA PROGRAM SHIRIKISHI
KWA KUJIFUNZA UZOEFU WA MASUALA MBALI MBALI NDANI YA NCHI WANACHAMA.
MKUTANO WA WAHASIBU HAO UNATARAJIWA KUWA NA WASHIRIKI ZAIDI YA 1000
WAKIWEMO WAHASIBU WAKUU 14 KUTOKA NCHI WANACHAMA NA WADAU WENGINE.
No comments:
Post a Comment