ZANZIBAR.
IMEELEZWA KUWA KUWEPO KWA PENCHENI YA JAMII HAPA
NCHINI KUTASAIDIA KUPUNGUZA UMASKINI KWA WANANCHI WAKE SAMBAMBA UKUAJI WA
UCHUMI.
HAYO AMEELEZWA
NA KATIBU MKUU WIZARA YA UWEZESHAJI USTAWI WA JAMII VIJANA WANAWAKE NA
WATOTO BI.ASHA ALI ABDALLA WAKATI AKIZUNGUMZA KATIKA KIKAO CHA PAMOJA KATI
YAWATENDAJI WAKUU WA WIZARA YAKE NA ALIEKUWA KATIBU MKUU WIZARA YA HIFADHI YA
JAMII MSHIKAMANO KITAIFA NA MABADILIKO YA KISEKTA KUTOKA MAURITIUS NDUGU
ANBANADEN VEERASAMY KWENYE UKUMBI WA WIZARA HIYO MWANAKWEREKWE .
KATIKA KUFIKIA HATUA HIYO SERIKALI IKO KATIKA
MCHAKATO WA KUWA NA SERA YA HIFADHI YA JAMII ILI MPANGO HUO UWEZO KUTEKELEZEKA
.
AMESEMA KUWA MPANGO HUO UTAKAPOANZA
UTAWEZA KUTOA PENCHENI KWA WOTE WAKIWEMO WAFANYAKAZI WA
SERIKALI , BINAFSI NA WAZEE WOTE WATAKAOFIKIA UMRI WA MIAKA 60.
BI. ASHA AMEFAHAMISHA KUWA TAYARI RASIMU
YA SERA HIYO IMESHAJADILIWA KATIKA NGAZI MBALIMBALI NA MUDA SI MREFU
ITAWASILISHWA KWA MAKATIBU WAKUU ILI KUWEZA KUTOA MICHANGO YAO .
AMEISHUKURU HELP AGE INTERNATIONAL KWA MCHANGO
WAKE KATIKA UTAYARISHAJI WA SERA YA HIFADHI YA JAMII PAMOJA NA SHUGHULI
KADHAA ZA WAZEE.
BW. VERASAMY AMBAE NI MTAALAM WA MFUMO WA
UTEKELEZAJI WA HIFADHI YA JAMII NCHINI MAURTIUS AMESEMA KUWA KATIKA
KUFIKIA MPANGO WA PENSHENI JAMII KILA MMOJA AWAJIBIKE KWA NAFASI I ALIYOPO NA
KUSHIRIKIANA KATIKA KAZI ILI KUFIKIA LENGO LILOKUSUDIA .
AMESEMA KUWA
SUALA LA UHAMASISHAJI WA JAMII NI MUHIMU KUZINGATIWA ILI UELEWA WA DHANA
HIYO UFAHAMIKE VIZURI KWA WOTE .
BW. ANBANADEN VEERASAMY AMBAE PIA NI KATIBU WA BARAZA
LA WAZEE NCHINI MAUNTIUS AKIWA
HAPA ZANZIBAR ANATARAJIWA KUWA NA MAZUNGUMZO NA UONGOZI WA WIZARA YA
FEDHA , WIZARA YA MAWASILIANO NA MIUNDO MBINU ,WIZARA YA AFYA, WIZARA YA
NCHI AFISI YA RAIS KAZI UTUMISHI WA UMMA , WIZARA YA ELIMU NA MAFUNZO YA
AMALI ,WIZARA YA NCHI AFISI YA RAIS TAWALA ZA MIKOA NA IDARA MAALIM NA UONGOZI
WA UNICEF ZANZIBAR.
No comments:
Post a Comment