PEMBA.
Wazazi na walezi wametakiwa kuwasomesha vijana
wao misingi ya dini ya kiislamu ili kudhibiti mmong’onyoko wa maadili kwa faida ya vizazi vya sasa na vya baadae.
Ushauri huo umetolewa na afisa wa elimu na Mafunzo ya Amali wa Mkoa wa kaskazini Pemba SAMAHATU SHEIKH Muhammed Nassor Salim wakati wa ghafla fupi ya mashindano ya Tahfidh qur ani yaliyoandaliwa na jumuiYa ya maendeleo ya WAnawake wa jimbo la Konde .
SHEIKH Nassor amesema KUWA iwapo watoto watajengwa vyema katika misIngi ya kidini vitendo vya udhalilishaji wa kijinsi ikiwemo ubakaji na ngono za jinsia moja zitaondoka katika jamiii.
Hata hivyo afisa huyo amesema KUWA nivyema kwa wazazi kutowa mshiirikianno ya pamoja na walimum wa madrasa ili,kwakufuatilia menendo ya watoto wao na kuwajengea uwezo walimu wa madrasa ili kukidhi mahitaji yao ya kilasiku,
Katika risala yao iliyosomwa na Khamisuu Juma Khamisi wamesema KUWA wamekabiliwa na changamoto mbali mbali ikiwemo uwelewa mdogo wa jamii pamoja na muamko mdogo katika kupinga udhalilishaji wa wanawake na watoto.
No comments:
Post a Comment