WILAYA YA MAGHARIBI
IMEELEZWA KUWA KUKOSEKANA KWA UFAHAMU WA SHERIA KUNACHANGIA KUONGEZEKA KWA
MSONGAMANO WA KESI KATIKA MAHAKAMA MBALIMBALI NCHINI.
WAKIZUNGUMAZA KATIKA KONGAMANO LA KUSHEHEREKEA SIKU YA
SHERIA DUNIANI BAADHI YA WANANCHI WAMESEMA KUWA KUTOLEWA KWA ELIMU YA
SHERIA KATIKA JAMII KUTASAIDIA KUPUNGUA KWA MALALAMIKO YA KESI ZA JINAI.
WAMEISHAURI
SERIKALI KWA KUSHIRIANA NA TASISI HUSIKA KUANZISHA MFUMO MAALUM WA KUINGIZA MITAALA YA SOMO LA
SHERIA KATIKA SKULI KWA LENGO LA KUJENGA UFAHAMU ZAIDI.
AIDHA WAMEFAHAMISHA KUWA UTENGENEZAJI WA SHERIA
UHUSISHE WANANCHI ILI KUONDOA MGOGORO KATIKA UTEKELEZAJI WAKE.
KWA UPANDE WAKE MWANASHERIA KUTOKA KITUO CHA HUDUMA ZA
SHERIA ZANZIBAR BI HARUSI MIRAJI
MPATANI AMESEMA KUWA TATIZO LA MUHALI NA UPOKEAJI WA RUSHWA
LIMEPELEKEA KUTOTEKELEZWA KWA DHANA YA UTAWALA BORA AMBAO NDIO UNAOCHANGIA
KUWEPO KWA HAKI ZA BINADAMU.
HATA HIVYO AMEELEZA KUWA WATENDAJI WA VYOMBO VYA SHERIA
WANAWAJIBU MKUBWA WA KUFUATA MAADILI YA KAZI KWA LENGO LA KUJENGA
HAKI NA KUIMARISHA MISINGI YA UTAWALA BORA KATIKA JAMII.
No comments:
Post a Comment