tangazo

tangazo

Sunday, February 8, 2015

SHIMO LA KIZA SEHEMU YA KWANZA SIMULIZI YA KWELI MIONGONI MWA YALIYOMKUTA KIJANA HAFIDH

SHIMO LA KIZA
SEHEMU YA KWANZA
SIMULIZI YA KWELI
jina langu kamili ni hafidh Hussein mwinyi nikiwa ni motto wa saba katika familia ya bibi mjane ajuza Hussein msingwa mzaramo wa kimbiji nilizaliwa miaka mingi iliyopita mara baada ya kufikia miaka nane baba yangu alifariki dunia nikabaki peke yangu na mama yangupamoja na dada zangu wawili ambao wao baada ya kufariki baba yangu yaani wetu wao walichukuliwa na ndugu na jamaa mbali mbali kwa ajili ya kulelewa ila mm binafsi sik...uwa tayari japo na udogo wa umri wangu kuishi mbali na mama yangu hichi ndicho kilichonifanya nizidi kumpenda mama yangu shida raha zote nilikuwa bega kwa bega na mama yangu kuhakikisha namfariji kwa hali na mali,nikasoma kwa shida na misukosuko huku nikishindia uji na kushindwa kujua kesho itakuwaje hadi ikafikia hatua nikaacha shule na kupelekwa kwa mjomba wangu dar kwa ajili ya kulelewa hali huko ilizidi kuwa ngumu mara baada ya mke wa mjomba wangu kutokuwa na mahaba ya dhati na wapwa wa mumewe ikanibidi nitororoke kurudi kwa mama yangu Zanzibar,nikarudi tena shule japo muda ulikuwa umeenda sana hali ambayo ilinifanya nisome na watu niliowazidi umri katika shule ya kwerekwe A,kisauni unguja,kiembe samaki na kumalizia kidato cha nne kwerekwe C mara baada ya matokeo ya kidato cha nne nikashindwa na kupata pasi za kuendelea na kidato cha tano na cha sita, nilikaa mwaka mzima nikifikiria nn nifanye vingi vilifikirika lakini uamuzi wangu wa mwisho na kutokana na ushiriki wangu katika jamii yangu na kupenda kuitumikia nikaamua kusoma fani ya uandishi wa habari kwa ngazi ya cheti mara baada ya kukamilisha masomo yangu ya uandishi na kufaulu kwa kiwango kizuri nikapelekwa katika masomo ya vitendo nikafanya vizuri katika redio ambayo nilifanya mazoezi ya vitendo na nikapata day worker hapo na sasa nina miaka mine hapo mwaka wa pili wa day worker yangu baba yangu mlezi akanitaka niowe maana alinambia nimekuwa sasa na napaswa kujitegemea sikuwa na pingamizi ila kama walivyo vijana wengine nilitamani niwe na nyumba yangu nzuri ndipo niowe lakini baba yangu kwa upendo na kunitakia utulivu aliniuliza wapokea kiasi gani kwa mwezi mara baada ya kumwambia akanambia piga maisabu ya kula kuvaa malazi mahitaji ya dharura itakuchukua miaka ishirini mpaka kujenga tena banda la vyumba viwili je? una uhakika wa kufika kesho ingia kwenye ndoa allah ndio mjuzi zaidi nakupa muda wa miezi mitatu unifahamishe wapi nikakuposee tukaishiana hapo nikaelekea nyumbani kupumzika.
nini kiliendelea ungana nami kesho katika simulizi yangu ya kusisimua mkasa wa kweli uliotokea kwenye maisha yangu mm binafsi itakuliza utanionea huruma lakini najivuania kuwa muislam ndio pekee utakaonifariji...............................

No comments:

Post a Comment