tangazo

tangazo

Sunday, February 1, 2015

RAIS WA UJERUMANI, JOACHIM GAUCK AMEWASILI NCHINI LEO USIKU KWA ZIARA YA KITAIFA YA SIKU TANO



DAR-ES-SALAAM.

RAIS WA UJERUMANI, JOACHIM GAUCK AMEWASILI NCHINI LEO USIKU KWA ZIARA YA KITAIFA YA SIKU TANO KWA MWALIKO WA RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA, DR  JAKAYA MRISHO KIKWETE.

KWA MUJIBU WA TAARIFA ILIYOTOLEWA NA KITENGO CHA MAWASILIANO YA SERIKALI KWA UMMA, WIZARA YA MAMBO YA NJE NA USHIRIKIANO WA KIMATAIFA RAIS GAUCK ATAPOKELEWA RASMI NA MWENYEJI WAKE RAIS KIKWETE IKULU MJINI DAR ES SALAAM NA KESHO  ATAKAGUA GWARIDE LA HESHIMA NA KUPIGIWA MIZINGA 21.
BAADA YA MAPOKEZI HAYO, RAIS GAUCK ATAFANYA MAZUNGUMZO YA FARAGHA NA RAIS KIKWETE YAKIFUATIWA NA MAZUNGUMZO RASMI.
AIDHA MARAIS HAO WATAKUTANA NA WAANDISHI WA HABARI.

BAADAYE  RAIS GAUCK ATAKUTANA NA WAFANYABIASHARA, NAKUTEMBELEA KANISA LA KILUTHERI LA AZANIA FRONT, ATAKUTANA NA WAWAKILISHI WA TAASISI ZA KIRAIA NA KUSHIRIKI DHIFA YA KITAIFA ITAKAYOANDALIWA NA MWENYEJI WAKE MHE. RAIS KIKWETE, IKULU.



RAIS GAUCK AMBAYE AMEONGOZANA NA MKE WAKE BIBI SCHADT, VIONGOZI WAANDAMIZI KUTOKA SERIKALI YA UJERUMANI NA UJUMBE WA WAFANYABIASHARA TISA, ATAONDOKA DAR ES SALAAM KUJA ZANZIBAR  KESHOKUTWA AMBAPO ATAFANYA MAZUNGUMZO RASMI NA RAIS WA ZANZIBAR DKT. ALI MOHAMMED SHEIN, KABLA YA KUSHIRIKI KATIKA MKUTANO WA KAMATI YA PAMOJA YA VIONGOZI WA DINI KUHUSU AMANI.
RAIS GAUCK PIA ATAKUTANA NA VIJANA KUTOKA UJERUMANI WANAOJITOLEA KATIKA PROGRAMU YA WELTWARTS HAPA ZANZIBAR.

RAIS GAUCK ATAONDOKA ZANZIBAR ALKHAMIS WIKI HII KUELEKEA MKOANI ARUSHA.

No comments:

Post a Comment