UONGOZI WA RADIO ADHANA UMEKUTANA NA
UONGOZI WA RADIO ALNOOR FM KATIKA OFISI ZA RADIO ALNOOR LEO HUKO MTONI
KIDATU KWA LENGO LA KUJENGA MASHIRIKIANO KATIKA SHUGHULI ZA RADIO ZA
KIISLAM.
WALIOKUTANA KATIKA MAZUNGUMZO HAYO NI PAMOJA NA MWENYEKITI WA BODI SH SALUM
ABDUSALAMY NA MKURUGENZI WA RADIO ADHANA KWA UPANDE MMOJA NA MKURUGENZI MKUU SH
NADIR MOHD MAHFOUDH NA NAIBU MKURUGENZI SH RASHID SALIM WA RADIO ALNOOR KWA
UPANDE WA PILI PAMOJA NA WATENDAJI WAKUU WA PANDE ZOTE MBILI, AMBAPO
WAMEKUBALIANA KUANGALIA MAENEO YA KUSHIRIKIANA NA KUSAIDIANA KATIKA
KUFIKIA LENGO LA RADIO ZAO LA KUELIMISHA NA KUUNGANISHA UMMA WA WAISLAMA.
AKIZUNGUMZIA UMUHIMU WA KUKUTANA NA KUBADILISHANA MAWAZO KATIKA UENDESHAJI WA
RADIO ZA KIISLAM MKURUGENZI MKUU WA RADIO ALNOOR SH NADIR MOHD AMESEMA RADIO
ZETU HIZI ZINA MATATIZO MENGI AMBAYO KWA KUSAIDIANA TUNAWEZA KUYATATUA HIVYO NI
VYEMA KUA PAMOJA KATIKA KAZI ZETU.
NAE MWENYEKITI WA BODI YA RADIO ADHANA SH SALUM ABDUSALAMY AMESEMA FIKRA HII
INAFAA KUFANYIWA KAZI HARAKA ILI KUKABILI KWA PAMOJA CHANGAMOTO ZILIZOPO
SAMBAMBA NA KUSAIDIA TAIFA KUHAMASISHA WANACHI KULINDA MAZINGIRA
YANAYOCHAFULIWA NA CHUPA ZA PLASTIC KWA KUANDAA VIPINDI VYA KUHAMASISHA
WANANCHI.
No comments:
Post a Comment