MKOWA WA KUSINI UNGUJA.
ENGEZEKO LA MAHOTELI YA KITALII KATIKA KIJIJI CHA MICHAMVI WILAYA YA KATI UNGUJA KUMEPELEKEA KIWANGO KIDOGO CHA UFAULU KWA WANAFUNZI WA SHEHIA HIYO.
AKIZUNGUMZA NA ADHANA FMA MWENYEKITI WA KAMATI YA SKULI YA MICHAMVI KAE BI:KHADIJA HASSAN HAJJI AMESEMA KUWA TOKEA KUSHAMIRI KWA HARAKATI ZA UTALII KATIKA KIJIJ HICHO KUMECHANGIA KUSHUKA KWA KIWANGO CHA MASOMO HASA KWA WANAFUNZI WA SEKONDARI.
AMEFAHAMISHA KUWA WANAFUNZI WALIO WENGI WAMEKUWA WAKIHADAIWA NA WAGENI WANAOKUJA KATIKA MAHOTELI HALI ILIYOCHANGIWA KUENGEZEKA KWA MIMBA ZA MAPEMA NA KUPELEKEA KUPOTEZA MUELEKEO WA MAISHA YAO.
AMESEMA JUMLA YA KESI TATU ZA UJAZITO ZIMERIPOTIWA KUTOKEA KATIKA SKULI HIYO KWA KIPINDI CHA MWAKA 2013 AMBAPO WAFANYAJI WOTE WA MAKOSA HAYO NI WAGHENI WANAKUJA KATIKA HOTELI HIZO.
KWA UPANDE WAKE SHEHA WA SHEHIA HIYO ND:ABEID JUYA HAJJI AMEKIRI KUWEPO KWA HALI HIYO AMBAPO AMESEMA INACHANGIWA NA BAADHI YA WAZAZI KWA KUTOKUWA NA USHIKIANO NA KAMATI YA SKULI YENYE LENGO LA KUSHUHULIKIA MATATIZO MBALIMBALI YA WANAFUNZI HAO.
AIDHA AMEFAFANUWA KUWA KUEPO KWA SEHEMU ZA STAREHE KUMEPELEKEA WANAFUNZI KUJISAHAU NA KUJIINGIZA KATIKA VITENDO VIOVU VINAVYOWASABAISHIA KUKATA MASOMO YAO.
SAMBAMBA NA HAYO AMESEMA KATIKA KUZIBITI TATTIZO HILO WANANCHI KWA KUSHIRIKIANA NA VIONGOZI WA MAJIMBO WAMEANZISHA MFUMO KUEKA KAMBI KATIKA SKULI HIYO KWA LENGO LA KUWAZIBITI WANAFUNZI WANAOTARAJIWA KUFANYA MITIHANI YA TAIFA ILI WAWEZE KUEPUKANA NA VISHAWISHI VYA MITAANI
No comments:
Post a Comment