oslo.
Zaidi ya watu 1000
wengi wao wakiwa waislamu wameunda mviringo na kulizunguka sinagogi nchini
Norway, kuonyesha umoja wao kufuatia mashambulizi kadhaa yaliyowalenga wayahudi
barani Ulaya.
Wakati waumini wa kiyahudi walipokuwa wakitoka
ndani ya sinagogi katika mji mkuu wa Norway Oslo, kulikuwa na shangwe wakati
vijana wa kiislamu walipowazingira kama ishara ya amani.
Warsha hiyo ilipangwa na vijana wa kiislamu na
kufanyika wiki chache baada ya kijana mmoja mzaliwa wa Denmark mwenye asili ya
Kiphalestina kuwaua watu wawili .
No comments:
Post a Comment