ZANZIBAR.
WANAFUNZI WA SKULI ZA SEKONDARI WANAOSOMA
MASOMO YA SAYANSI NA WALIMU WAO TANZANIA WAMESISITIZWA KUONGEZA JUHUDI KATIKA
MASOMO YAO NA KUFANYA TAFITI ZITAKAZOSAIDIA KUGUNDUA MATATIZO YA
AFYA YANAYOIKABILI NCHI HIVI SASA IKIWEMO MARADHI YA KENSA.
RAIS WA JUMUIYA YA WATAALAMU WA FANI MBALI MBALI
ZA AFYA ZANZIBAR (BLUE HEALTH ORGANISATION) GORA FAKI HAJI AMETOA USHAURI HUO
KATIKA SEMINA YA KUELIMISHA TATIZO LA MARADHI YA KENSA ILIYOWASHIRIKISHA
BAADHI YA WANAFUNZI WA MASOMO YA SAYANSI WA SKULI ZA SEKONDARI KATIKA
SKULI YA HAILESSELASSIE.
AMEWAELEZA WANAFUNZI HAO KWAMBA KENSA NI
MIONGONI MWA MARADHI HATARI YANAYOSUMBUA WANANCHI WENGI TANZANIA NA IDADI KUBWA
YA WATU WANAOPATA MARADHI HAYO HUPOTEZA MAISHA.
RAIS HUYO WA BLUE HEALTH ORGANISATION
AMEONGEZA KUWA ASILIMIA 66 YA WAGONJWA WA KENSA WALIOFIKA OCEAN
ROAD KUPATIWA MATIBABU NI WANAWAKE NA ASILIMIA 24 WANAUME NA HIYO
INAONYESHA WANAWAKE WANASUMBULIWA ZAIDI NA MARADHI HAYO.
AMESEMA
KUWA PAMOJA NA KUWA HAKUNA SABABU RASMI INAYOPELEKEA KUPATA
KENSA MOJA KWA MOJA LAKINI AMESEMA MATUMIZI YA BIDHAA ZINAZOTOKANA NA TUMBAKU,
UTUMIAJI WA POMBE NA MPANGALIO USIORIDHISHA WA CHAKULA UNACHANGIA KUPATA TATIZO
LA MARADHI HAYO.
AMEWATAKA WANANCHI KUJIEPUSHA NA VIASHIRIA
VINAVYOWEZA KUPELEKEA KUPATA KENSA NA KUWA NA UTARATIBU MZURI WA CHAKULA
IKIWEMO KUTUMIA ZAIDI MATUNDA NA MBOGA ZA MAJANI.
AMEWASHAURI WATU KUJENGA TABIA YA KUFANYA
UCHUNGUZI WA AFYA ZAO MARA KWA MARA NA KUWA NA TAHADHARI WANAPOPATA
TATIZO LA UVIMBE KATIKA MIILI YAO.
AMEWAHAKIKISHIA WANANCHI KUWA BLUE HEALTH
ORGANISATION ITAENDELEZA LENGO LA KUTOA TAALUMA YA MASUALA YA AFYA KWA
MAKUNDI MBALI MBALI ILI WAWEZE KUFAHAMU SABABU ZINAZOPELEKEA MARADHI NA
NJIA ZA KUJIEPUSHA NAYO.
SEMINA HIYO ILIWASHIRIKISHA WANAFUNZI WA SKULI ZA
SEKONDARI LUMUMBA, BENBELLA, HAMAMNI NA BAADHI YA WALIMU WA SKULI HIZO
WANAOSOMESHA MASOMO YA SAYANSI.
No comments:
Post a Comment