ZANZIBAR.
SEREKALI YA MAPINDUZI YA ZANZIBAR IMESEMA KUWA WANANCHI KWA KUSHIRIKIANA NA VIONGOZI WANA NAFASI
KUBWA YA KULINDA NA KUENDELEZA USHIRIKIANO KATIKA MALEZI YA WATOTO WANAOISHI
KATIKA MAZINGIRA MAGUMU.
HAYO YAMEELEZWA
LEO NA WAZIRI WA NCHI OFISI YA MAKAMO WA KWANZA WA RAISI FATMA
ABDUL-HABIB FEREJI WAKATI AKIFUNGUA MKUTANO MKUU WA JUMUIYA YA KUSAIDIANA
KWA HALI NA MALI(JUKUHAMA) KATIKA UKUMBI WA EACROTANAL MJINI ZANZIBAR.
AMESEMA KUWA SUALA LA USHIRIKIANO NI MUHIMU KWA
LENGO LA KUIKOMBOA JAMII KATIKA WIMBI LA MMONG’ONYOKO WA MADILI AMBAO HUCHANGIA
KUTOPATIKANA KWA MAENDELEO YA HARAKA.
HATA HIVYO
WAZIRI HUYO AMEFAHAMISHA KUWA
WAZAZI WATAKAPOENDELEZA MALEZI YA PAMOJA WATAWEZA KUIHAMASISHA JAMII
KUONDOKANA NA VITENDO VIOVU IKIWEMO UDHALILISHAJI WA WANAWAKE NA WATOTO
WANAOISHI KATIKA MZAINGIRA MAGUMU.
AKIZUNGUMZIA SUALA LA MATUMIZI YA DAWA ZAKULEVYA
AMESEMA KUWA VIJANA WENGI WAMEATHIRIWA NA UTUMIAJI WA MADAWA HIZO JAMBO AMBALO
LINALOWAPELEKEA VIJANA HAO KUISHI KATIKA HALI NGUMU.
KWA UPANDE WAKE KATIBU WA JUMUIYA HIYO ABDUL-RAHMANI
SULTANI AMESEMA KUWA LENGO LA KUANZISHA JUMUIYA HIYO NI KUWASAIDIA WATOTO
YATIMA NA WASIOJIWEZA PAMOJA NA KUWAHAMASISHA VIJANA KUSHIRIKI KATIKA KAZI
ZA AMALI ILI ZIWEZE KUWASAIDIA KWA KUWAEPUSHA NA MAZINGIRA
HATARISHI WANAPOMALIZA ELIMU YA LAZIMA.
NAO VIJNA WALIOSHIRIKI KATIKA MKUTANO HUO WAMESEMA KUWA
KUWEPO KWA JUMUIYA HIZO KUTAWEZESHA VIJANA KUJIKINGA NA VIKUNDI HATARISHI
KATIKA MITAA AMBAVYO HUWASABABISHIA KUFANYA MAMBO MAOVU.
No comments:
Post a Comment