DOHA.
MAKAMU WA KWANZA WA RAIS WA ZANZIBAR MAALIM SEIF SHARIF HAMAD AMEISHAURI
SERIKALI YA QATAR KUANGALIA UWEZEKANO WA KUSHIRIKIANA NA ZANZIBAR KATIKA
KUENDELEZA SEKTA YA NISHATI NCHINI.
MAALIM SEIF AMETOA USHAURI HUO WAKATI AKIZUNGUMZA NA WAZIRI WA NISHATI NA
VIWANDA WA QATAR DR. MOHAMMED SALEH AL-SADA, IKIWA NI MWENDELEZO WA ZIARA YAKE
NCHINI HUMO.
AMESEMA KUWA ZANZIBAR IKIWA MIONGONI MWA NCHI ZINAZOENDELEA, BADO
INAKABILIWA NA CHANGAMOTO NYINGI IKIWEMO YA UPATIKANAJI WA UMEME WA UHAKIKA
AMBAPO KWA SASA INATEGEMEA NISHATI HIYO KUTOKA TANZANIA BARA.
AMESEMA KUWA WAKATI UMEFIKA KWA ZANZIBAR KUWA NA VYANZO VYAKE VYA UMEME, NA
KWAMBA SERIKALI IMO KATIKA MKAKATI WA UPATIKANAJI WA VYANZO MBADALA VYA UMEME,
ILI KUHAKIKISHA KUWA HUDUMA HIYO INAKUWA YA UHAKIKA.
AMEMUELEZA WAZIRI HUYO NA UJUMBE WAKE KUWA LICHA YA ZANZIBAR KUTOKUWA NA
MITO YA KUZALISHA NISHATI HIYO, LAKINI INAWEZA KUPATIKANA KUPITIA NGUVU ZA JUA
NA UPEPO AMBAPO BAADHI YA TAFITI ZIMESHABAINI UWEZEKANO WA UPATIKANAJI WAKE.
HIVYO AMESEMA KUWA QATAR IKIWA NCHI YENYE UZOEFU MKUBWA KATIKA SEKTA YA
NISHATI, INAYO FURSA YA KUSHIRIKIANA NA ZANZIBAR ILI KUHAKIKISHA KUWA VISIWA
VYA UNGUJA NA PEMBA VINAKUWA NA VYANZO VYAKE VYA UMEME NA KUIFANYA HUDUMA HIYO
KUWA YA UHAKIKA.
MAALIM SEIF AMETAJA CHANGAMOTO NYENGINE INAYOIKABILI ZANZIBAR KUWA NI
UKOSEFU WA AJIRA KWA VIJANA, HALI INAYOTISHIA MUSTAKBALI WA MAENDELEO YA VIJANA
HAO AMBAO WENGI WAO TAYARI WAMEPATA ELIMU YA SEKONDARI HADI KUFIKIA VYUO VIKUU.
KATIKA MAZUNGUMZO HAYO WAZIRI WA NISHATI NA VIWANDA WA QATAR DR. MOHAMMED
SALEH AL-SADA, AMEISHAURI SERIKALI YA MAPINDUZI YA ZANZIBAR KUWEKA UTARATIBU
MZURI KWA WAWEKEZAJI WA SEKTA MBALI MBALI, IKIWA NI PAMOJA NA KUIMARISHA
MIUNDOMBINU YAKE.
UCHUMI WA QATAR UNATEGEMEA ZAIDI SEKTA YA MAFUTA NA GESI ASILIA AMBAYO
HUCHANGIA ZAIDI YA ASILIMIA 70 YA PATO LA TAIFA HILO LINALOKUA KWA KASI
KIUCHUMI.
No comments:
Post a Comment