MAKAMU WA PILI WA RAIS WA ZANZIBAR BALOZI SEIF ALI IDDI AMEIPONGEZA
SERIKALI YA MAREKANI KUPITIA SHIRIKA LAKE LA MISAADA YA MAENDELEO LA US AID KWA
JITIHADA ZAKE ZA KUISAIDIA ZANZIBAR KATIKA MIPANGO YAKE YA KUTAFUTA MBINU ZA
KUWA TAYARI KWA KUKABILANA NA MAAFA WAKATI WOWOTE YATAPOTOKEZEA.
BALOZI SEIF AMETOA PONGEZI HIZO WAKATI AKIFUNGUA RASMI MAFUNZO YA
SIKU TANO KUHUSU ZOEZI LA KUKABILIANA NA MAAFA ZANZIBAR YANAYOFANYIKA KATIKA
UKUMBI WA HOTELI YA ZANZIBAR BEACH RESORT MAZIZINI NJE KIDOGO YA MJI WA
ZANZIBAR.
AMESEMA KUWA ZANZIBAR IMEKUWA NA
HISTORIA KUBWA YA MAJANGA MBALI MBALI YALIYOWAHI KUIKUMBA NA
KUSABABISHA MAAFA MAKUBWA YATAYOENDELEA KUKUMBUKWA NA VIZAZI VYA SASA NA
VIJAVYO.
AMESEMA KUWA MAREKANI IMEKUWA
MSHIRIKA MKUBWA KATIKA KUSAIDIA HARAKATI MBALI MBALI ZA MAENDELEO YA MIUNDO
MBINU YA MAWASILIANO YA BARA BARA, HUDUMA ZA AFYA NA USTAWI WA JAMII WA
ZANZIBAR JAMBO AMBALO LIMEKUWA LIKILETA FARAJA KWA WANANCHI WALIO WENGI HAPA
NCHINI.
BALOZI SEIF ALIFAHAMISHA KWAMBA JUHUDI ZA ZANZIBAR KATIKA KUJIWEKA TAYARI
KUKABILIANA NA MAAFA YOYOTE YATAKAYOWEZA KUTOKEA ZIMEKUJA KUFUATIA MAJANGA
TOFAUTI YALIYOWAHI KUTOKEA KAMA MARADHI YA KOLERA, AJALI ZA VYOMBO VYA
USAFIRI WA BAHARINI NA MAJANGA YA MOTO AMBAYO YAMESABABISHA VIFO VYA WATU
KADHAA.
ALIFAHAMISHA KWAMBA ZANZIBAR IKIWA MIONGONI MWA MATAIFA MACHANGA
DUNIANI INAWAJIBIKA KUIMARISHA IDARA YAKE YA MAAFA KWA KUSHIRIKIANA NA TAASISI
ZA ULINZI, AFYA NA MAWASILIANO ILI KUONA HUDUMA ZA KUKABILIANA NA MAAFA NCHINI
ZINAPATIKANA KWA UBORA UNAOKUSUDIWA.
MAFUNZO HAYO YA SIKU TANO KUHUSU ZOEZI LA KUKABILIANA NA MAAFA
ZANZIBAR YANAYOFANYIKA KATIKA UKUMBI WA MIKUTANO WA HOTELI YA ZANZIBAR
BEACH RESORT YAMESHIRIKISHA WAWAKILISHI WA TAASISI ZA ULINZI, MAAFA, UTAWALA,
PAMOJA NA WATAALAMU WA AFYA KUTOKA NCHI MBALI MBALI DUNIANI.
No comments:
Post a Comment