zanzibar.
SEREKALI YA MAPINDUZI YA ZANZIBAR IMESEMA KUWA ITAENDELEA KUTOA USHIRIKIANO NA TAASISI MBALI MBALI KWA LENGO LAKUIMARISHA HUDUMA ZA
AFYA.
AKIZUNGUMZA KATIKA KILELE CHA SIKU YA SARATANI DUNIANI
NAIBU WAZIRI WA AFYA MAHMOUD THABIT KOMBO AMESEMA KUWA SEREKALI KWA KUSHIRIKIANA
NA WADAU WA AFYA IMEKUSUDIA KUANZISHA VITENGO VYA MARADHI MBALI MBALI ILI
KUWAONDOLEA USUMBUFU WANANCHI KUFUATA HUDUMA KATIKA NCHI JIRANI.
HATA HIVYO WAZIRI HUYO AMEBAINISHA KUWA WIZARA YA AFYA
KUPITIA MFAMASIA MKUU INAENDELEA NA JITIHADA ZAKUFUATILIA TIBA ZA MARADHI
YASIYOAMBUKIZA YAKIWEMO KENSA,KISUKARI NA UTOAJI ELIMU KWA WANANCHI.
KWA UPANDE WAKE DAKTARI BINGWA WA MARADHI MBALI MBALI
NCHINI MSAFIRI MARIJANI AMESEMA KUWA WAGONJWA 100 HUJITOKEZA KILA MWAKA KATIKA
MAENEO YA UNGUJA NA PEMBA HALI INAYOASHIRIA KUONGEZEKA KWA MARADHI HAO.
HATA HIVYO AMESEMA KUWA KUKOSEKANA KWA BAADHI YA VITENDEA
KAZI IKIWEMO DAWA YA MIONZI YAKUPIMIA WAGONJWA HAO KUMEPELEKEA WAGONJWA
KUPELEKWA TANZANIA BARA JAMBO AMBALO LINASABABISHA KUONGEZEKA KWA UGONJWA HUO
NCHINI.
SIKU YA SARATANI DUNIANI HUADHIMISHWA KILA IFIKAPO TAREHE
MWEZI WA PILI YA KILA MWAKA NA KAULI MBIU YA MWAKA HUU NI SULUHISHO LA SARATANI
LIMO NDANI YA UWEZO WETU.
No comments:
Post a Comment