tangazo

tangazo

Friday, February 13, 2015

WAUMINI WA DINI YA KIISLAM NCHINI WAMETAKIWA KUPENDA NA KUCHUKIA KWA AJILI YA MAAMRISHO YA DINI YAO



ZANZIBAR.
WAUMINI WA DINI YAKIISLAM KOTE NCHINI WAMETAKIWA KUPENDA NAKUCHUKIA VITU MBALI MBALI KWA KUZINGATIA QUR-AN NA SUNNA ZA MTUME MUHAMMAD S.A.W.

WITO HUO UMEOLEWA LEO NA SAMAHATU SHEIKH MUHAMMED ALI WAKATI AKITOA KHUTBA 2 ZA SALA YA IJUMAA KATIKA VIUNGA VYA MSIKITI WA JUMUIYA YA FIISABILLAH TABLIGH MARKAZ FUONI WILAYA YA MAGHARIBI UNGUJA.

AMEWASISITIZA WAISLAM KUACHA TABIA YAKUPENDA VITU VISIVYOPENDWA NA M/MUNGU S.W ILI KUPATA RADHI ZAKE.

AIDHA KHATIBU HUYO AMEWATAKA WAISLAM KUHAKIKISHA KUWA CHOCHOTE WANACHOPENDA KUPENDA KWA AJILI YA MOLA WAO.

AKIZUNGUMZIA SIKU POTOFU YA WAPENDAO YA VALANTIN DAY ALIM HUYO AMEWAKUMBUSHA WAISLAM KUJIEPUSHA NAYO ILI KUEPUKA GHADHABU KUTOKA KWA MOLA WAO.

IBADA YA HIYO YA SWALA YA IJUMAA KATIKA VIUNGA VYA MASJID FIISABILILAH TABLIGH MARKAZ FUONI MIGOMBANI IMEHUDHURIWA NA WAISLAM WA FUONI NA MAENEO JIRANI.

No comments:

Post a Comment