Zanzibar.
Mjumbe wa Bodi ya
Mfuko wa Bima ya Afya Tanzania Ezekiel Olouchi AMEISHAURI Serikali ya Mapinduzi
ya Zanzibar KUUNGANISHA Taasisi zake na mfuko HUO ili KUWAPA fursa
WAFANYAKAZI kupata huduma bora na Ya
uhakika ya afya inayotolewa na Hospitali mbali mbali hapa Nchini.
Olouch AMETOTOA Ombi
hilo wakati akizungumza na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali
Iddi Ofisini kwake Vuga Mjini Zanzibar.
NDUGU Ezekiel
aliyeuongoza ujumbe wa Viongozi wanne wa Bodi hiyo ya Bima ya Afya walikuwepo
Zanzibar kukutana na viongozi wa Taasisi mbali mbali za Muungano ambazo
wafanyakazi wake ni wanachama wa Mfuko huo kuangalia huduma zinazotolewa
kupitia mfuko huo.
AMEsema KUWA licha ya sheria ya Bima ya Afya
KUTOtumikA Zanzibar zipo baadhi ya
Taasisi na wafanyakazi wa umma wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar walioonyesha
NIA ya kutaka kujiunga na mfuko huo wakiwa na lengo la kutaka kuIMARISHA afya
zao.
Bwana Olouchi
aMEsema kUWA mfanyakazi yeyote aliye mwanachama wa mfuko huo wa Bima ya
Afya ana haki ya kutibiwa katika muda wote wa maisha yake LICHA YAKUstaafu kazi katika Taasisi Aliyokuwa
akiifanyia kazi.
Mjumbe huyo wa Bodi
ya Mfuko wa Bima ya Afya Tanzania ameushauri uongozi wa Hospitali ya Umma
Zanzibar kujitahidi kujijengea miundo mbinu imara ya vifaa itakayotoa
ushawishi kwa Tasisi zenye wanachama wa mfuko huo kupeleka wafanyakazi wao
kutibiwa katika Hospitali hizo.
Naye Makamu wa Pili
wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi aMEsema kUWA licha yaSerikali ya
Mapinduzi ya Zanzibar kuweka huduma za Afya bila ya malipo mara baada ya
Mapinduzi ya mwaka 1964 haizuii watu
binafsi kujiunga na Mfuko wa Bima ya Afya.
Balozi Seif aMEsema KUWA
wazo la Uongozi huo wa Bodi ya Mfuko wa Bima ya Afya litazingatiwa ipasavyo na
Serikali ili kuona namna ya kuzipa fursa Taasisi zake kuamuwa kujiunga na mfuko
huo kulingana na sheria iliyopo.
Jumla ya shilingi
Bilioni 1.1 zimekusanywa na Hospitali binafsi kutokana na michango ya huduma za
afya zinazotolewa na Wanachama wa Mfuko wa Bima ya Afya tokea mwezi Aprili
Mwaka 2014 wakati Hospitali za Serikali ni Shilingi Milioni Mia 1.7 PEKEE.
No comments:
Post a Comment