ZANZIBAR.
CHAMA CHA WANANCHI CUF, KIMESEMA KUWA KINAUNGA MKONO TAMKO
LILILOTOLEWA NA UMOJA WA KATIBA YA WANANCHI (UKAWA) HIVI KARIBUNI LA KUSUSIA
KURA YA MAONI KUHUSU KATIBA MPYA INAYOPENDEKEZWA.
AKITANGAZA UAMUZI HUO KATIKA MKUTANO WA HADHARA WA UZINDUZI WA KAMATI ZA
UCHAGUZI ZA CHAMA HICHO ULIOFANYIKA KATIKA VIWANJA VYA MNAZI MMOJA ZANZIBAR,
KATIBU MKUU WA CUF MAALIM SEIF SHARIF HAMAD AMESEMA KUWA WAMEAMUA KUFANYA HIVYO
KWA MADAI KUWA TARATIBU ZILIZOTUMIKA KUANDIKA KATIBA HIYO NI BATILI NA
HAZIKUBALIKI.
AKIZUNGUMZIA KUHUSU KAMATI ZA UCHAGUZI, MAALIM SEIF AMEWATAKA WAJUMBE WA
KAMATI HIZO KUFANYA KAZI KWA UMAKINI NA UADILIFU, NA KUWATAHADHARISHA WAJUMBE
WASIOWEZA KAZI HIYO KUACHIA NGAZI MAPEMA, ILI KUEPUKA KUCHUKULIWA HATUA ZA
KISHERIA.
AMESEMA KUWA KUZINDULIWA KWA KAMATI HIZO NI HATUA MOJA MUHIMU YA MKAKATI WA
CHAMA HICHO KUELEKEA UCHAGUZI MKUU WA OKTOBA MWAKA HUU, NA KWAMBA UZINDUZI HUO
UMEFANYIKA KWA MAFANIKIO.
AMESEMA KUWA KAZI KUBWA YA KAMATI HIZO KATIKA NGAZI ZOTE ZA MATAWI,
MAJIMBO, WILAYA NA TAIFA, NI KUHAKIKISHA USHINDI MKUBWA KWA CHAMA HICHO KATIKA
UCHAGUZI MKUU UJAO.
KATIKAM UZINDUZI HUO WA KAMATI ZA UCHAGUZI MAALIM SEIF AMEKABIDHI VIFAA
MBALI MBALI VYA KUFANYIA KAZI KATIKA ZONI ZA CHAMA HICHO, WILAYA NA MAJIMBO,
VIKIWEMO MAGARI 14, VESPA 50 NA VIFAA VYA OFISINI.
MAPEMA AKIZUNGUMZA KATIKA MKUTANO HUO, MSHAURI WA MIKAKATI WA KATIBU MKUU
WA CUF MANSOUR YUSSUF HIMID, AMESEMA CHAMA HICHO KINAKUSUDIA KUUNDA SERIKALI
ITAKAYOTHAMINI UTU WA WATU WENGINE, DHAMA AMBAYO ILIKUWA MIONGONI MWA DHAMIRA
ZA MUASISI WA MAPINDUZI YA ZANZIBAR MAREHEMU MZEE ABEID AMANI KARUME.
UZINDUZI WA KAMATI HIZO ULIKWENDA SAMBAMBA NA MATEMBEZI YA WANAKAMATI
KUTOKA MAJIMBO YOTE UNGUJA NA PEMBA, YALIYOANZIA VIWANJA VYA MALINDI HADI MNAZI
MMOJA.
No comments:
Post a Comment