tangazo

tangazo

Wednesday, February 4, 2015

WAnafunzi watu wazima (46) wamaliza Diploma ya Sayansi ya Jamii, Afya na Mazingiara katika chuo cha Sayansi ya Afaya Mbweni kutoka Unguja na Pemba



zanzibar.

WAnafunzi watu wazima (46) waliomaliza Diploma ya Sayansi ya Jamii, Afya na Mazingiara katika chuo cha Sayansi ya Afaya Mbweni  kutoka Unguja na Pemba wameahidi kuendeleza umoja na mashirikiano kati yao na walimu wao hadi kufikia hatua Ya juu zaidi katika kada hiyo na kuleta ufanisi zaIdi makazini mwao. 

Ahadi hiyo imetolewa na mwakilishi wa wanAfunzi hao NdUGU RASHID ABEID KATUNDU huko katika Ukumbi wa afisi za Meli Nne Saccos ,katika tafrija na hafla maalum waliyowaandalia walimu wao pamoja na kujipongeza kwa hatua ya kumaliza ngazi ya Diploma katika fani hiyo na kuwaletea maendeleo makubwa ya kielimu katika jamii nchini. 

Wamesema KUWA kutokana na umri wao, majukumu yao ya kazi na kushughulikia familia wameweza kukabiliana na changamoto nyingi zilizokaribia kuwakatisha tamAa walimudu kumaliza na kufanikisha masomo yao vizuri. 

Aidha  NdUGU  Katundu amewashukuru  walimu wao hao kwa msaada, jitihada na mashirikiano makubwa kati yao na kueleza kuwa katika maendeleo yao walimu wao hao wAlichangia kwa kiasi kikubwa hadi kupata mafanikio yao kwa kutumia mbinu bora za ufundishaji watu wazima. 

amewaomba wananchi wengine watu wazima waliopo makazini na mitaani katika jamii kutokata tamAa bali nao wajiunge kwa wingi katika chuo cha Sayansi ya Afya, Mbweni  NA vyuo  vyengine ili kujiendeleza na kutekeleza agizo la Serikali la watu wazima kujiendeleza kielimu. 

Nae mwalimu OTHMAN BAKAR MOH’D kutoka Pemba kwa niaba ya walimu wenzake amewashukuru wanafunzi hao kwa ukarimu wao na kueleza kuwa waMEweza  kumudu vizuri masomo yao yatakayowasaidia katika kuleta mabadiliko makubwa katika kazi zao. 

aKITOA MAOMBI KWA NIAMBA YA  walimu WA Kisiwani Pemba MWALIMU OTHMAN AMEIomba Serikali kupitia Wizara ya Afya na Chuo cha Sayansi ya Afya, Mbweni kuendeleza aina hiyo yautoaji taaluma kwa watu wazima na  kufungua tawi kwa ajili ya wananchi kisiwani Pemba. 

TaAluma iliyotolewa kwa wanafunzi hao ni pamoja na masuala ya Uongozi, Afya ya Jamii na Mazingira. 

No comments:

Post a Comment