tangazo

tangazo

Saturday, February 21, 2015

MISIKITI ITUMIKE KUWAUNGANISHA WAISLAM ASEMA DK SHEIN



WILAYA YA KUSINI.
RAIS WA ZANZIBAR ALHAJ DK. ALI MOHAMED SHEIN  AMEWATAKA  WAUMINI DINI YAKIISLA KUITUMIA MISIKITI KWA KUWAUNGANISHA.
DR SHEIN AMETOA WITO HUO LEO WAKATI AKIFUNGUA MSIKITI WA KIONGONI MAKUNDUCHI WILAYA YA KUSINI UNGUJA.
ALHAAJ SHEIN AMESEMA KUWA HAITOKUWA VYEMA KUSIKIA MIZOZO IKIWA NI PAMOJA NA KUGOMBANIA UONGOZI WA MSIKITI MIONGONI MWA VIONGOZI KATIKA MISIKITI.
AMESEMA KUWA LICHA YA KUWA BAADHI YA WAKATI WAPO WANAOKHAFILIKA NA KUFANYA HIVYO AMBAPO ALHAJ DK. SHEIN ALIELEZA KUWA IMANI YAKE NI KUWA WAUMINI WATAFUATA NYAYO ZA MASHEHE NA MAULAMAA WALIOPITA KATIKA KUFUATA MATENDO MEMA.
AIDHA, DK. SHEIN AMESISITIZA KUWA MSIKITI HUO PAMOJA NA MADRASA ALIZOZIFUNGUA ZIWE NI CHEMCHEM YA ELIMU MBALI MBALI IKIWA NI PAMOJA NA USOMAJI KURAN, FIKHI NA TAALUMA NYENGINE ZA DINI, MALEZI NA IMANI.
DK. SHEIN AMESEMA KUWA KIONGONI IMETOA WATU MBALI MBALI WENYE MAARIFA MAKUBWA KAMA MAREHEMU SHEIKH IDRISA ABDUL WAKIL AMBAYE ALITOA MCHANGO MKUBWA KATIKA MAENDEO YA NCHI.
SAMBAMBA NA HAYO, DK. SHEIN ALIWASISITIZA WAUMINI KUENDELEA KUHIMIZANA KUHUSU  UMUHIMU WA KUENDELEZA AMANI ILIYOPO KWA MANUFAA YAO NA VIZAZI VILIVYOPO NA KUWATAKA WAZAZI KUTOCHOKA KUSIMAMIA MALEZI YA WATOTO NA KUWAELEKEZA KATIKA MAADILI MEMA SAMBAMBA NA MIENENDO INAYOZINGATIA UTAMADUNI NA MAFUNDISHO YA DINI.
ALHAJ DK. SHEIN AMESEMA KUWA UJENZI WA MSIKITI NA MADRASA NI MASUALA YA KHERI NA YENYE UMUHIMU KATIKA KUUENDELEZA UISLAMU.
MAPEMA KABLA YA UFUNGUZI WA MSIKITI HUO, ALHAJ DK. SHEIN ALIFUNGUA MADRASATUL TAWHEED ILIYOPO HAPO HAPO KIONGONI MAKUNDUCHI.
WAKATI HUO HUO, ALHAJ DK. SHEIN ALIZINDUA MADRASATUL MUZDALIFA AL-QADIRIA SHAFII, HUKO MZURI MAKUNDUCHI NA KUELEZA KUWA KUNA HAJA YA KUIMARISHA MASHIRIKIANO BAINA YA WAZAZI, WALIMU NA  NA JAMAII YOTE KWA JUMLA KATIKA KUWAEPUSHA WATOTO NA WANAWAKE KATIKA VITENDO VYA UDHALILISHAJI.

No comments:

Post a Comment