tangazo

tangazo

Monday, February 9, 2015

Zaidi ya nyumba elfu tatu na mia nne zinatarajiwa kupigwa dawa ya mbu wa malaria



Zanzibar      
Zaidi ya nyumba elfu tatu na mia nne zinatarajiwa kupigwa dawa ya mbu wa malaria katika maeneo ya visiwa  vya unguja na pemba kwa lengo la kumaliza mbu wanaosambaza ugonjwa huo.
Akizungumza na waandishi wa habari meneja wa kitengo cha kumaliza malaria Zanzibar Abdallah Suleiman  amesema kuwa wizara ya afya kupitia kitengo cha malaria imekusudia kuendelea na zoezi la upigaji dawa katika shehia kumi na saba ambazo bado zina mambukizi ya ugojwa huo.
Amefahamisha kuwa moja katika mikakati ya kumaliza malaria Zanzibar ni pamoja na kupiga dawa majumbani  sambamba na ugawaji wa vyandarua  ila jamiiiweze kupambana na ugonjwa huo.
Akizitaja wilaya zitakazo husika na zoezi hilo ni pamoja na wilaya ya kati,kusini, magharibi  na wilaya ya kaskazini A na B kwa unguja ambapo kwa kisiwa cha pemba ni wilaya ya micheweni,chake chake, wete na mkoani.
Sambamba na hayo amewataka  wananchi kutoa ushirikiano katika zoezi hlo na kufuata taratibu ili kuepuka madhara ya upigaji wa dawa hiyo.

No comments:

Post a Comment