ZANZIBAR.
Wizara ya Habari, Utamaduni, Utalii na Michezo
Zanzibar imetia saini mkataba wa makubaliano ya kuanzishwa kwa ofisi ya
uwakala wa Utangazaji Utalii wa Zanzibar Nchini India.
AKITIA saini
Mkataba huo katika ukumbi wa Wizara hiyo iliyopo Kikwajuni Mjini Zanzibar Katibu Mkuu wa Wizara hiyo DR Ali Mwinyikai
AMESEMA KUWA uanzishwaji wa ofisi ya utalii nchini India ni utekelezaji
wa malengo yaliyopangwa na Serikali ya
Mapinduzi ya Zanzibar iliyopo madarakani kwa upande wa sekta ya Utalii kwa
lengo la kuitangaza zaidi Zanzibar kiutalii.
Aidha Katibu huyo amesema kuwepo kwa ofisi za Utalii
nchini India KUtasaidia kujenga uhusiano mzuri na wa kudumu baina ya Zanzibar
na wadau mbalimbali wa Utalii walioko nchini India jambo ambalo linakosekana
katika masoko yaliyopo hivi sasa ispokua soko la ItalY.
DR Mwinyikai amefahamisha kuwa kutokana na hali hiyo
Serikali ya MAPINDUZI YA Zanzibar imeamua kuongeza nguvu na kubadilisha
mikakati ya utafutaji wa masoko mengine ikiwa ni pamoja na yale yanayochipukia
yakiwemo ya Nchi za China, India, Urusi na Uturuki.
Nae mkurugenzi mtendaji wa kampuni ya Jihil
Enterprises ya India ambae pia ni mzaliwa wa Zanzibar anaeishi Mumbai India
NCHINI INDIA Jilesh H. Babla amesema
KUWA ameamua kuwa wakala wa Utalii wa Zanzibar Nchini India kwa lengo la kuitangaza
Zanzibar kiutalii kwani Zanzibar ina vivutio vingi vya Kiutalii zikiwemo
Fukwe,Mandhari Nzuri na sehemu za kihistoria.
Amesema ameamua maamuzi ya kizalendo kuwa Wakala wa
Zanzibar Nchini India kwani hadi sasa hakuna wazalendo wanaoishi nje ya Nchi
waliyojitikeza kufanya kazi hiyo pamoja na kuvitaka vyombo vya habari Zanzibar
kufikisha ujumbe uliyo sahihi kwa wananchi juu ya Utalii wa Zanzibar ili kukuza
Utalii wa nchi na hatimae kupelekea kukua kwa uchumi wa nchini.
Nae Mwenyekiti wa Bodi ya Kamisheni ya Utalii
Zanzibar Dr. Ahmada Khatib amesema KUWA wazo la kuwa na Ofisi ya Utalii Nchini
India lilitokana na matokeo ya ziara rasmi ya Rais wa Zanzibar aliyoifanya
Nchini China na India tarehe 27/05/2013 hadi 02/06/2013 ambayo ilijumuisha
Mawaziri mbalimbali wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.
UTIAJI
SAINI HUO ULIKUWA KATI YA Katibu
Mkuu wa Wizara ya Habari DR Ali Mwinyikai na Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya
JIHIL ENTERPRISES ya India Nd. Jilesh
No comments:
Post a Comment