ZANZIBAR.
Idara ya Ardhi na Mazingira inatarajia kufanya
Uzinduzi wa Mfumo wa Mtandao wa Upatikanaji Taarifa za Ardhi Zanzibar (Zanzibar
Land Information Service) (ZALIS) itakayosaidia upatikanaji wa taarifa sahihi
za Ardhi nchini.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Idara hiyo
uzinduzi huo utafanyika KESHO katika jengo la Ardhi liliopo Forodhani
Mjini Zanzibar.
TAARIFA HIYO imeONGEZA KUWA mtandao huo wenye
teknolojia rahisi itakayosaidia kwa kiasi kikubwa upatikanaji wa Khabari na
taarifa zote za Ardhi ikiwemo usajili, utambuzi, upimaji, uhaulishaji eneo,
kijografia, mipaka na kuongeza ufanisi wa shughuli zote ardhi kwa kiasi
kikubwa.
mfumo wa ZALIS utarahisisha upatikanaji wa taarifa na
takwimu zinazohitajika Kijamii na Kiuchumi juu ya masuala ya Ardhi na kuzifanya
shughuli hizo kuwa rahisi na nyepesi zaidi.
Aidha Serikali ya Finland kupitia Wizara yake ya
Mambo ya Nchi za Nje imekuwa KUisaidia Zanzibar katika masuala mbalimbali
ikiwemo Maji, Mazingira, Misitu pamoja na Ardhi kwa zaidi ya miaka 10 hadi
sasa.
Taarifa hiyo imefahamisha kuwa maendeleo ya usajili
wa Ardhi yamekuwa yakiendelea vizuri nchini ambapo hadi sasa jumla ya viPANDE
34,000 vimeshapatiwa usajili wa kudumu.
Mfumo wa ZALIS umefadhiliwa na Serikali ya Finland
ambao umegharimu zaidi ya shilingi milioni 100 ambapo mgeni rasmi katika
Uzinduzi huo anatarajiwa kuwa Balozi wa Finland nchini Tanzania Bi. Sinnika
Antilla.
No comments:
Post a Comment