tangazo

tangazo

Friday, February 13, 2015

KUPUNGUZA IDADI YA VIFO VYA MAMA WAJAWAZITO NA WATOTO WACHANGA NI MIONGONI MWA MASUALA MUHIMU AMBAYO BADO YANAHITAJI KUZINGATIWA



ZANZIBAR.
RAIS WA ZANZIBAR DK. ALI MOHAMED SHEIN AMESEMA SUALA LA KUIMARISHA MAISHA YA JAMII NA KUPUNGUZA IDADI YA VIFO VYA MAMA WAJAWAZITO NA WATOTO WACHANGA NI MIONGONI MWA MASUALA MUHIMU AMBAYO BADO YANAHITAJI KUZINGATIWA KWA KINA KATIKA MPANGO WA MIAKA MITANO IJAYO WA MAENDELEO ENDELEVU YA UMOJA WA MATAIFA (UN).
DK. SHEIN AMESEMA HAYO LEO WAKATI ALIPOKUTANA NA UJUMBE WA WAKUU WA MASHIRIKA YA UMOJA WA MATAIFA WENYE OFISI ZAO HAPA NCHINI AMBAO WALIFIKA IKULU MJINI ZANZIBAR KUZUNGUMZA NA RAIS WAKIONGOZWA NA MWAKILISHI MKAAZI WA UMOJA WA MATAIFA TANZANIA BWANA ALVARO RODRIGUEZ.
DK. SHEIN AMESEMA KUWA LICHA YA SERIKALI YA MAPINDUZI YA ZANZIBAR KUPIGA HATUA KUBWA KATIKA  MALENGO YA MILENIA, SUALA LA KUPUNGUZA IDADI YA VIFO VYA MAMA WAJAWAZITO NA WATOTO WACHANGA LIMEBAKI KUWA CHANGAMOTO KUBWA KWA SERIKALI AMBAPO HATA HIVYO JUHUDI ZA MAKUSUDI ZIMEENDELEA KUCHUKULIWA NA MAFANIKIO YANAONEKANA.
KATIKA MAZUNGUMZO HAYO, DK. SHEIN AMESEMA KUWA CHANGAMOTO KUBWA KATIKA KUFIKIA MALENGO YA MILENIA KWENYE ENEO HILO INATOKANA NA UPUNGUFU WA WATAALAMU HAPA NCHINI SAMBAMBA NA UFAHAMU MDOGO WA JAMII KUHUSU UMUHIMU WA WAZAZI KUJIFUNGULIA KWENYE VITUO VYA AFYA.
HATA HIVYO, AMESEMA KUWA SERIKALI YA MAPINDUZI YA ZANZIBAR IMEENDELEA KUCHUKUA JUHUDI KUBWA KATIKA KUKABILIANA NA CHANGAMOTO HIYO IKIWA NI PAMOJA NA KUONGEZA IDADI YA MADAKTARI NA WATAALAMU WANAOTOA HUDUMA ZA AFYA KUTOKA MADAKTARI 3,634 MWAKA 2010 HADI KUFIKIA 4,618 MWAKA JANA AMBAPO KWA MUJIBU WA MADAKTARI WOTE WA SASA DAKTARI MMOJA ANATOA HUDUMA KWA WATU 9,708.
AIDHA, ALISEMA KUWA SERIKALI YA MAPINDUZI YA ZANZIBAR IMEKUWA IKITOA TAALUMA KWA JAMII KUHUSIANA NA UMUHIMU WA AKINAMAMA KUJIFUNGUA HOSPITALINI SAMBAMBA NA
KUONDOA AINA ZOTE ZA MALIPO KWA AKINAMAMA WANAOJIFUNGUA KWENYE HOSPITALI ZA SERIKALI.
AMEONGEZA KUWA TATIZO LA AJIRA KWA VIJANA, KUIMARISHA MAISHA, LISHE BORA NA USTAWI WA JAMII HASA KWA WATOTO,  WANAWAKE NA MAKUNDI YALIYO KATIKA MAZINGIRA HATARISHI NI MIONGONI MWA CHANGAMOTO ZILIZOPO AMBAZO BADO JUHUDI ZA MAKUSUDI  ZINAENDELEA KUCHUKULIWA NA SERIKALI NA KUSISITIZA HAJA YA KUENDELEA KUUNGWA MKONO.
AMESEMA KATIKA KUKABILIANA NA TATIZO LA AJIRA, SERIKALI IMEANZISHA MFUKO MAALUM WA UWEZESHAJI KIUCHUMI KWA LENGO KUWASAIDIA VIJANA, LAKINI ONGEZEKO KUBWA LA VIJANA WANAOMALIZA VYUO VIKUU LIMELETA CHANGAMOTO KWA SERIKALI.
DK. SHEIN AMEYASHUKURU MASHIRIKA YOTE YA UMOJA WA MATAIFA KWA MISAADA YAO MBALI MBALI INAYOTOA KWA ZANZIBAR NA KUELEZEA MATUMAINI YAKE KWAMBA MASHIRIKA HAYO YATAENDELEA KUFANYAKAZI KWA PAMOJA NA SERIKALI KATIKA UTEKELEZAJI WA MALENGO MAPYA KWA KIPINDI CHA MIAKA MITANO IJAYO.
NAYE KIONGOZI WA UJUMBE HUO MRATIBU MKAAZI WA SHIRIKA LA MPANGO WA MAENDELEO LA UMOJA WA MATAIFA BWANA ALVARO RODRIGUEZ  UMOJA WA MATAIFA KUPITIA MASHIRIKA YAKE YALIOPO HAPA NCHINI  UTAENDELEA KUIUNGA MKONO ZANZIBAR KATIKA KUENDELEZA NA KUIMARISHA SEKTA ZA MAENDELEO 
BWANA RODRIGUEZ ALISEMA KUWA CHANGAMOTO ZOTE ZILIZOJITOKEZA KATIKA UTEKELEZAJI WA MALENGO YA MILENIA ZINATARAJIWA KUENDELEA KUPATIWA UFUMBUZI KWENYE MPANGO UPYA UJAO AMBAO UTAJUMUISHA MASUALA YA MAENDELEO YA UCHUMI, USTAWI WA JAMII,  UTAWALA BORA, PAMOJA NA DEMOKRASIA NA MAENDELEO.
PAMOJA NA HAYO, MWAKIKILISHI MKAAZI HUYO ALIPONGEZA JUHUDI ZINAZOCHUKULIWA NA SERIKALI YA MAPINDUZI YA ZANZIBAR CHINI YA UONGOZI WA DK. SHEIN KATIKA KUFIKIA MALENGO YALIYOWEKWA SAMBAMBA NA MASHIRIKIOANO MAKUBWA INAYOTOA KWA MASHIRIKA YA UN HAPA NCHINI.

No comments:

Post a Comment