tangazo

tangazo

Monday, February 9, 2015

MFUMKO WA BEI UMEPUNGUA TANZANIA NA AFRIKA MASHARIKI



DAR-ES-SALAAM.

OFISI YA TAIFA YA TAKWIMU IMESEMA KUWA MFUMUKO WA BEI WA TAIFA KWA MWEZI JANUARI, 2015  UMEPUNGUA HADI KUFIKIA ASILIMIA 4.0 KUTOKA ASILIMIA 4.8 YA MWEZI DESEMBA, 2014 KUTOKANA NA KUENDELEA KUPUNGUA KWA KASI YA BEI YA BIDHAA NA HUDUMA MBALIMBALI NCHINI.

AKITOA TAARIFA YA MFUMUKO HUO MJINI DAR ES SALAAM, MKURUGENZI WA TAKWIMU ZA JAMII WA OFISI YA TAIFA YA TAKWIMU EPHRAIM KWESIGABO AMESEMA KUWA KUPUNGUA KWA MFUMUKO WA BEI KATIKA MAENEO MBALIMBALI NCHINI KUMESABABISHWA NA KUPUNGUA KWA KASI YA BEI YA BIDHAA ZA VYAKULA NA  NA BIDHAA NYENGINE.

AMESEMA KIWANGO CHA MABADILIKO YA HARAKA YA BEI ZA BIDHAA NA HUDUMA ZOTE ZINAZOTUMIWA NA KAYA KIMEONYESHA KUPUNGUA KATIKA MAENEO MBALIMBALI NCHINI KIKIHUSISHA BEI YA MAHINDI, UNGA WA MAHINDI , NDIZI ZA KUPIKA NA MUHOGO.

AIDHA KWESIGABO AMEELEZA KUWA BIDHAA ZISIZO ZA VYAKULA ZILIZOCHANGIA KUPUNGUA KWA MFUMUKO WA BEI NCHINI NI PAMOJA NA MAFUTA YA TAA ASILIMIA 8.4, DIZELI ASILIMIA 10.2, PETROLI KWA ASILIMIA 6.8 NA  GESI YA KUPIKIA KWA ASILIMIA 2.9.

AKITOA UFAFANUZI KUHUSU  KIWANGO CHA MABADILIKO YA KASI YA BEI ZA BIDHAA NA HUDUMA ZOTE ZINAZOTUMIWA NA KAYA BINAFSI KWA KIPIMO CHA MWEZI KATI YA MWEZI DESEMBA 2014 NA JANUARI 2015 , AMESEMA KUWA MWEZI JANUARI UMEKUWA NA ONGEZEKO LA ASILIMIA 1.0 IKILINGANISHWA NA ONGEZEKO LA ASILIMIA 2.0 LA MWEZI DESEMBA , 2014.

KWA UPANDE WA MFUMUKO WA BEI WA MWEZI NOVEMBA 2014 KATIKA NCHI ZA AFRIKA MASHARIKI AMESEMA UNA MWELEKEO UNAOFANANA , KENYA UKIPUNGUA  NA KUFIKIA  ASILIMIA 5.53 KWA MWEZI JANUARI 2015, KUTOKA ASILIMIA 6.02 ZA MWEZI DESEMBA 2014, UGANDA  MFUMUKO WA BEI KWA MWEZI JANUARI 2015 UMEPUNGUA HADI ASILIMIA 1.3 KUTOKA ASILIMIA 1.8 ZA MWEZI DESEMBA 2014.

No comments:

Post a Comment