tangazo

tangazo

Wednesday, February 4, 2015

Imeleezwa kuwa asasi ya kiraia zina nafasi kubwa katika kufanikisha udhibiti wa uharibifu wa mazingira unaotokana na mabadiliko ya Tabianchi .



PEMBA.

Imeleezwa kuwa  asasi ya kiraia zina nafasi kubwa katika kufanikisha udhibiti wa uharibifu wa mazingira unaotokana na mabadiliko ya Tabianchi .

Hayo yameelezwa na Mkuu wa Wilaya ya Wete KISIWANI Pemba Hassan Khatib Hassan wakati akizungumza na Uongozi wa Jumuiya ya Maendeleo ya Jimbo la Mtabwe.

Amesema kuwa katika kufanikisha hilo asasi za kiraia zinatakiwa kuwa mstari wambele kuwaelimisha wananchi athari za mabadiliko ya Tabia nchi yanayotokea siku hadi siku.

Mkuu huyo wa Wilaya ameitaka Jumuiya hiyo kuhakikisha kUWA  maeneo ya wazi ambayo yameathirika kwa kukatwa miti ovyo yanarejeshwa katika hadhi yake kwa kupandwa miti.

Aidha amewataka Viongozi wa Jumuiya hiyo kufanya kazi zao kwa mujibu na katiba yao na kuacha kuyaingiza masuala ya Kisiasa wakati wa utekelezaji na ufuatiLIaji wa kazi za Jumuiya hiyo .

Naye Diwani wa Wadi ya Mtambwe NDUGU Hamad Mjaka  Bakar amesema kuwa lengo Jumiya hiyo ni kutoa elimu ya utunzaji wa mazingira pamoja kutatua kero zao. .

MNAENDELEA  KUSKILIZA  TAARIFA  YA  KHABARI  KUTOKA  REDIO   ADHANA   FM MASJID JUMUIYA RAHALEO ZANZIBAR.

No comments:

Post a Comment