DODOMA.
KAMPUNI YA MS SHIMOJA YENYE MAKAO MAKUU YAKE KATIKA
JIMBO LA MICHIGAN NCHINI MAREKANI IKO MBIONI KUTAKA KUANZISHA KITUO CHA
MATANGAZO YA TELEVISHENI MJINI DAR ES SALAAM NCHINI KITAKACHOTOA HUDUMA NDANI
YA UKANDA WA AFRIKA MASHARIKI.
MKURUGENZI WA KAMPUNI HIYO AMBAE PIA NI BALOZI WA HESHIMA
WA TANZANIA NCHINI MAREKANI DR. ROBERT SHUMAKE ALIELEZA HAYO WAKATI AKIZUNGUMZA
NA MAKAMU WA PILI WA RAIS WA ZANZIBAR BALOZI SEIF ALI IDDI OFISINI KWAKE KATIKA
JENGO LA MSEKWA NDANI YA VIUNGA VYA BUNGE LA JAMUHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
MJINI DODOMA.
DR. SHUMAKE AMESEMA
KUWA LICHA YA KWAMBA MATANGAZO YA TELEVISHENI YANACHUKUWA SEHEMU KUBWA
YA BURDANI LAKINI KITUO HICHO KITALENGA ZAIDI KUTOA VIPINDI WA ELIMU
VITAKAVYOWASAIDIA WANANCHI NA HASUSAN WANAFUNZI WA ELIMU YA MSINGI, SEKONDARI
NA VYUO VIKUU AFRIKA MASHARIKI.
AMESEMA KUWA MIPANGO INAANDALIWA NA KAMPUNI HIYO KATIKA
KUYASHIRIKISHA MAKAMPUNI YA MITANDAO YA MAWASILIANO DUNIANI YA GOOGLE NA
MICROSOFT ILI KUONA ELIMU INAYOKUSUDIWA KUFIKISHWA KWA UMMA KUPITIA MATANGAZO
YA KITUO HICHO YANAFANIKIWA KWA KIWANGO KIKUBWA.
DR. SHUMAKE ALIFAHAMISHA KWAMBA MPANGO HUO UNAKUSUDIWA
KWENDA SAMBAMBA NA ULE UTAKAOANDALIWA NA KAMPUNI HIYO WA KUWAPATIA MAFUNZO
VIJANA WAPATAO 50,000 KUTOKA BARA LA AFRIKA KATIKA JIMBO LA MICHIGAN NCHINI
MAREKANI.
ALISEMA HATUA HIYO INAKUSUDIA KUWAJENGEA UWEZO WA AJIRA
VIJANA HAO KATIKA FANI YA UJASIRI AMALI UTAKAOWAPA FURSA NZURI YA KUFANYA
KAZI KATIKA TAASISI NA MASHIRIKIA YOYOTE YA KITAIFA NA KIMATAIFA.
NAYE MAKAMU WA PILI WA RAIS WA ZANZIBAR BALOZI SEIF ALI
IDDI ALIMSHUKURU DR. ROBERT SHUMAKE PAMOJA NA KAMPUNI YAKE KWA UAMUZI HUO
WA BUSARA UTAKAOWEZESHA KUISAIDIA PIA SERIKALI KATIKA MAPAMBANO DHIDI YA UHABA
WA AJIRA NCHINI.
BALOZI SEIF ALISEMA SERIKALI ZOTE MBILI ILE YA
JAMUHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA NA YA MAPINDUZI YA ZANZIBAR ZIMEWEKA MILANGO
WAZI KWA TAASISI NA MASHIRIKA YA KITAIFA NA KIMATAIFA KUWEKEZA MIRADI YAO KWA
KUTUMIA RASILMALI ZILIZOPO NCHINI ILI KUSAIDIA NGUVU ZA KIUCHUMI NA
KUPUNGUZA UKALI WA MAISHA.
MAKAMU WA PILI WA RAIS WA ZANZIBAR ALIMSHAURI MKURUGENZI
HUYO WA KAMPUNI YA MS SHIMOJA YA NCHINI MAREKANI KUANGALIA FURSA NYINGI
ZAIDI ZA UWEKEZAJI ZILIZOPO NCHINI TANZANIA AMBAZO KAMPUNI YAKE INAWEZA
KUONGEZA UWEKEZAJI ZAIDI.
No comments:
Post a Comment