tangazo

tangazo

Monday, February 23, 2015

DK JAKAYA AHIDI KUZISAIDIA KAYA 40 AMBAZO NYUMBA ZAO ZIMEHARIBIWA NA MVUA CHALINZE



MKOA  WA PWANI
Rais WA JAMHURI YA MUUNGANO Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete AMEahidi kuzisaidia kAya 40 ambazo nyumba zao ziliharibiwa vibaya na mvua kubwa iliyoambatana na upepo mkali wiki iliyopita huko Chalinze,wilayani Bagamoyo Mkoani Pwani.


Katika ziara hiyo Rais Kikwete ambaye alikuwa amefuatana na mkewe mama Salma Kikwete alikagua Skuli ya msingi Chalinze, Ofisi ya CCM, na nyumba kadhaa za wanakijiji, ambazo ziliharibiwa vibaya na mvua hizo na kujeruhi baadhi ya wanavijiji walioangukiwa na nyumba zao.

Mvua kubwa iliyoambatana na upepo mkali wiki liyopita iliharibu kabisa majengo nane katika kata ya Chalinze, ambapo kuta zilibomoka mabati kuezuliwa na upepo mkali, na miti kuangukia nyumba na kujeruhi wana kijiji kadhaa ambao walitibiwa katika hospitali ya Tumbi.
Kaya 47 kutoka vijiji vya Msoga na Tonga ziliathirika na mkasa huo.

No comments:

Post a Comment